Imaam Ibn Rajab: Sha'baan: Swiyaam Za Sha’baan Kulinganisha Na Swiyaam Za Miezi Mitukufu Na ‘Ibaadah Nyinginezo

 

Swiyaam Za Mwezi Wa Sha’baan Kulinganisha Na Swiyaam Za Miezi Mitukufu

Na ‘Ibaadah Nyinginezo

 

Imaam Ibn Rajab (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Na Imaam Ibn Rajab (Rahimahu Allaah) amesema:

 

''Swawm katika Sha’baan ni bora kuliko Swawm katika masiku matakatifu (ambayo ni Dhul Qa'dah, Dhul-Hijjah, Muharram na Rajab zilizotajwa katika Suwrah At-Tawbah Aayah ya 36), na Swawm zilizo bora ni zile (zitambulikazo) ambazo ziko karibu na Ramadhwaan, kabla au baada. Hadhi na daraja ya Swawm hizi ni kama ya zile za Swalaah za Sunnah za Rawaatib, ambazo huswaliwa kabla na baada ya Swalaah za fardhi na ambazo huwa ni vijazilio vya upungufu wa zile Swalaah za fardhi. Na hali kama hiyo ndiyo ile ile ya Swawm zitambulikazo ambazo huwa kabla na baada ya Ramadhwaan, Kama ambavyo Swalaah za Sunnah za Rawaatib zilivyo bora kuliko Swalaah zingine za kujitolea (za Sunnah), na hivyo ndivyo Swawm zitambulikazo (zilizo katika miezi) ya kabla na baada ya Ramadhwaan zilivyo bora kuliko Swawm nyinginezo.''

 

 

[Latwaaif Al-Ma'aarif fiyma li Mawaasim Al'Aam Minal Wadhwaaif].

 

 

 

Share