Imaam Ibn Baaz: Ramadhwaan: Mambo Ambayo Yanampasa Mu’takif Katika Kutekeleza I’tikaaf Yake

Mambo Ambayo Yanampasa Mu’takif Katika Kutekeleza I’tikaaf Yake

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) 

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nini Kimpasacho Mu’takif Katika Kutekeleza I’tikaaf Yake?

 

 

JIBU:

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amejibu:

 

Ni juu ya Mu’takif atimize I’tikaaf yake na ajishughulishe na dhikru-Allaah na ‘ibaadah wala asitoke isipokuwa kwa haja anayohitaji mwana Aadam kama kwenda msalani kukojoa na kadhaalika, au akihitaji chakula ikiwa hakupata uwezekano wa mwenye kumtayarishia chakula basi atoke kwa ajili ya haja yake hiyo wala haijuzu kwa mwanamke amwendee mumewe hali ya kuwa yeye mke yuko kwenye I’tikaaf. 

 

Na kadhaalika Mu’takif haimpasi kumwendea mkewe, na lililo bora kwake ni kwamba asizungumze na watu lakini akiwa ametembelewa na baadhi ya ndugu zake au mwanamke ametembelewa na baadhi ya mahaarim wake akazungumza nao (wanaume) au akazungumza na wanawake wenzake, basi hakuna neno.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/440)]

 

 

Share