Shaykh Fawzaan: Imaam Kuomba Du’aa Baada Ya Swalaah Kwa Sauti Na Maamuma Kuitikia Aamiyn

 

Haikuthibiti Imaam Kuomba Du’aa Baada Ya Swalaah Kwa Sauti

Na Maamuma Kuitikia "Aamiyn"

 

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

Shaykh Swaalih Fawzaan  amesema:

 

 “Na inapendeza kujihirisha Tahliyl, Tasbiyh, Tahmiyd na Takbiyr baada ya kila Swalaah lakini isiwe kwa sauti ya pamoja. Kila mmoja anasome peke yake. Baada ya kumaliza adhkaar hizi, kila mmoja anaomba kwa siri kile  anachotaka. Hakika ni kuwa du’aa baada ya ‘Ibaadah na hizi adhkaar tukufu inaleta uwezekano mkubwa zaidi wa kujibiwa. Haifai kudhihirisha du’aa bali anaifanya kwa sauti ndogo, kwani kufanya hivyo ni karibu zaidi na ikhlaasw na unyenyekevu na mbali zaidi na riyaa. Ama kwa yale yanayofanywa na baadhi ya watu katika baadhi ya nchi kwa kuleta du’aa ya pamoja baada ya Swalaah kwa sauti kubwa au Imaam aombe na maamuma waitikie “Aamiyn”, hii ni bid‘ah inayochukiza kwani haijapokewa kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa alikuwa anaposwalisha watu na baada ya kumaliza Swalaah akiomba kwa njia hii. Hakufanya hivyo katika Swalaah ya Alfajiri, wala Alasiri, wala Swalaah nyinginezo, wala hakupendeza hilo yeyote miongoni mwa Maimamu”

 

[Al-Mulakhkhaswu Al-Fiqhiyy Mj. 1, uk. 154 – 160].

 

 

 

Share