Imaam Ibn Al-Qayyim: Kuwapongeza Makafiri Katika Sherehe Zao Ni Haraam

 

Kuwapongeza Makafiri Katika Sherehe Zao Ni Haraam

 

Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah)

 

 

www.alhidaaya.com

 

  

 Imaam Ibn Al-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

 

 Kuwatakia kheri makafiri katika mwenendo wao ni haraam kwa makubaliano ya wengi, kama ilivyo haraam kuwatakia kheri katika sherehe zao na funga zao kwa mfano kusema: “Kila la kheri katika sherehe” au “Nakutakia sherehe njema”, na mengineyo. Hata kama yule anayesema haya ameepushwa na ukafiri, lakini bado imekatazwa. Ni kama vile kumpa hongera mtu kwa kuuhami msalaba, au zaidi ya hivyo. Ni kama mfano wa dhambi iliyo kubwa sawa na kumpa hongera mnywaji ulevi, au kumuua mtu, au kuwa na mahusiano ya kinyama, na mengineyo. Wengi miongoni mwa wasio na taadhima ya dini yao wanaangukia kwenye kosa hili; hawakai kufikiria ubaya wa vitendo vyao. Yeyote anayempa hongera mtu kwa kutovukwa na adabu au bid’ah au ukafiri amejiweka wazi na laana pamoja na ghadhabu za Allaah.”

 

[Imaam Ibn Al-Qayyim: Ahkaam Ahl adh-Dhimmah]

 

 

 

 

Share