Shaykh Fawzaan: Mwenye Hedhi Kugusa Qur-aan Au Aayah Katika Simu Za Mkononi

 

Mwenye Hedhi Kugusa Qur-aan Au Aayah Katika Simu Za Mkononi

 

Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya mwanamke mwenye hedhi kugusa maneno ya Qur-aan ambayo yamo katika simu za mkononi?

 

 

JIBU:

 

(Hukmu ya Qur-aan iliyomo katika) Simu za mkononi, si (sawa) kama Qur-aan yenyewe (Msahafu) bali hiyo ni dijitali; kwa hiyo anaruhusiwa kuibeba au kuishika.

 

 

[Sharh ‘Umdatil-Fiqh, kanda Namba 7, swali namba 24]

 

 

Share