Imaam Ibn Taymiyyah: Rajab: Swalaatur-Raghaaib Haina Asili Bali Ni Bid’ah

 

Swalaatur-Raghaaib Haina Asili Bali Ni Bid’ah

 

Imaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

“Ama Swalaatur-Raghaaib haina asili bali hiyo ni bid’ah, hivyo haifai kuswaliwa kwa (Swalaah ya) jamaa wala mtu kuiswali pekee. Imethibiti katika Swahiyh Muslim kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza kuufanya usiku wa Ijumaa kuwa ni makhsusi kwa Qiyaam (kisimamo cha kuswali), na wala  (kufanya makhsusi) siku ya Ijumaa kwa Swawm. Na aathar iliyotajwa humo wamekubaliana ‘Ulamaa kwamba mna uongo na mawdhwuw’ na hakuna hata Salaf mmoja wala Maimaam walioitaja kabisa.” [Majmuw’ Fataawaa (23/132)]

 

Share