Shaykh Fawzaan: Ramadhwaan: Nasiha Kuomba Du'aa Unapokaribia Mwezi Wa Ramadhwaan

 

Nasiha Kuomba Du'aa Unapokaribia Mwezi Wa Ramadhwaan

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

SWALI:

 

Nini Nasiha yenu kuhusu kukaribia mwezi wa Ramadhwaan?

 

JIBU:

 

 

“Ni waajib kwa Muislamu kumuomba Allaah Amfikishe Ramadhwaan au Amsaidie katika Swiyaam zake na Qiyaam (kisimamo cha usiku kuswali), na katika ‘amali zake, kwa sababu ni fursa ya uhai wa Muislamu.  Anasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

((مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ))    البخاري ومسلم

Amesema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Atakayefunga Ramadhwaan kwa iymaan na kutaraji malipo ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al Bukhaariy na Muslim]

 

Na pia,

 

((مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ)) رواه البخاري 37 ومسلم 759   

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayesimama kuswali Ramadhwaan kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Basi Muislamu afurahie kwa kukurubia Ramadhawan na ashangalie na aupokee kwa furaha na  atumie fursa katika uttifu wa Allaah katika usiku wake kwa Qiyaam (kisimamo cha kuswali usiku)  na mchana wake kwa Swiyaam na kusoma Quraan na kumdhukuru Allaah, kwani hayo ni chumo la faida kwa Muislamu. 

 

Ama wale ambao inapokaribia Ramadhwaan wanaandaa vipindi vya ufisadi  na  misalsalaat  (michezo ya tamthilia  ya televisheni) na  na mishindano (ya michezo) ili wawashughulishe Waislaumu, basi hao ni askari wa mashaytwaan na mashaytwaan ni askari wao. Hivyo Muislamu atahadhari nao na ajiepusha nao. Ramadhwaan si wakati wa upuuzi wala mchezo wala misalsalaat, wala) mashindano (ya michezo) ya   zawadi na upotezaji wa wakati.

 

[Mawqi' Ar-Rasmiy li-Ma'aaliy Shaykh Swaalih bin Fawzaan]

 

 

 

 

 

Share