Kuku Wa Kuchoma Wa Sosi Ya HP

Kuku Wa Kuchoma Wa Sosi Ya HP

  
Vipimo  

Kuku (miguu)  - 5 pounds (vipande 20-25) 

Vitu vya sosi (sauce)

Kitunguu saumu/thomu na Tangawizi iliyosagwa  3 Vijiko vya supu

Chumvi - Kiasi

Sosi ya soy (soy sauce) - 2 vijiko vya supu

HP sauce -  3 vijiko vya supu               

Siki au ndimu -  3 Vijiko vya supu

Pilipili manga - 1 kijiko cha supu

Nyanya ya kopo - 1 kijiko cha chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
 
1.   Msafishe kuku kwa siki au bizari ya manjano kukata harufu.
 
2.   Mtie katika treya ya kuchomea, weka chumvi kisha mchome (bake) kwa muda kiasi hadi karibu na kuwiva.
 
3.   Mwaga maji yatakayotokeza kwa ajili ya kumchoma.
 
4.   Changanya vitu vyote vya sosi (sauce) na tia katika kuku  umchanganye vizuri na sosi  hiyo.
 
5.   Mrudishe katika jiko kwa kumchoma sasa kwa moto wa juu
    (grill) hadi awive vizuri na ageuke rangi na tayari kuliwa.

 

 

 

Share