Skip to main content

Sharbati Ya Embe Maziwa Na Mtindi

Sharbati Ya Embe Maziwa Na Mtindi

Vipimo

Maembe yaliyoiva - 2

Mtindi (yogurt) - 2 Vikombe vya chai

Maziwa mazito (Condensed Milk) - kikopo 1

Barafu - 12 vipande

Arki au rose essence - matone

Namna Ya Kutayarisha

  1. Menya maembe kisha ukate kate vipande.
  2. Weka vipimo vyote isipokuwa  kwenye mashine ya kusagia (blender).
  3. Saga hadi ilainike.
  4. Mimina kwenye gilasi sharbati iko tayari

 Bis-swihhah wal-hanaa (kunywa kwa siha na kuburudika)