Burger Ya Samaki Tuna

Burger Ya Samaki Tuna

Vipimo

Vibati vya samaki tuna - 2

Mikate ya duara (buns) - 10 – 12

Mahindi yaliyokwishapikwa -  ½ kikombe

Matango - 2

Mayonaise - 3 vijiko vya kulia

Chumvi - ¼ kijiko cha chai   

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai                            

Zaytuni (olives) au vitungule/vinyanya vidogo vya round

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katakata matango slesi ndogo.
  2. Kamua samaki wa tuna, kisha changanya pamoja na mahindi, matango, mayonnaise, chumvi na pilipili manga.
  3. Kata mikate (buns) katika sehemu mbili kisha weka mjazo wa tuna katika kila mkate mmoja.
  4. Weka zaytuni moja katika kijiti cha mshikati kisha chomeka katika burger.
  5. Panga katika sahani ikiwa tayari kuliwa.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

 

Share