Fajita - (Fa-hee-ta) Ya Nyama Ng’ombe (Spanish)

Fajita - (Fa-hee-ta) Ya Nyama Ng’ombe (Spanish)

Vipimo

Slaisi ya Steki ya nyama ng’ombe (veal slices) - 2 Lb (1 Kilo)

Mikate ya Tortilla (takriban nchi 7-8) - 12

*Salsa yake ya tayari au tayarisha - 1 kikombe cha chai

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilochunwa (grated) - 5 chembe

Kitunguu majani a (spring onions) - 3 miche

Nyanya/tungule - 2

Saladi la uwa (salad ice-berg) - ¼

Pilipili boga la kijani - 1

Pilipili boga jekundu - 1

Mafuta - ¼ kikombe

Masala yake* - 2 vijiko vya supu

Ndimu - 1

Chumvi - kiasi

Jibini ya mazorella (cheese) - 2 vikombe vya chai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 1. Kata kata nyama vipande vidogo dogo kiasi viwe virefurefu.
 2. Changanya na thomu, chumvi, na masala yake na ndimu uache katika friji ikolee kwa muda wa masaa hivi.
 3. Katakata nyanya, kitunguu majani, saladi, pilipili mboga weka kando.
 4. Kuna (Grate) jibini ikiwa sio ya tayari weka kando.
 5. Weka karai katika moto, tia mafuta, kisha kaanga nyama hadi iive na iwe kavu. Tia mapilipili mboga uliyokatakata changanya.
 6. Epua weka kando
 7. Panga mikate ya Tortilla katika treya ya oveni kisha gawa nyama kote sawasawa, tia saladi, nyanya, kitunguu.
 8. Nyunyizia salsa ya tayari na jibini iliyokunwa kisha pasha moto kidogo kwa kuweka katika oveni moto wa juu (Grill) kama dakika 5 tu.
 9. Epua na kunja kama picha.

*Salsa  ikiwa huna Ya tayari

Vipimo

Mafuta - 2 vijiko vya supu

Kitunguu - 1

Nyanya - 4

Nyanya ya kopo - 2 vijiko vya supu

Nanaa iliyokatwakatwa (chopped) - 2 misongo (bunch)

Kotmiri (coriander) iliyokatwakatwa (chopped) - 2 misongo (bunch)

Chumvi - kiasi

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

Namna ya Kutayarisha  Na Kupika Salsa

 1. Katakata kitunguu, kaanga katika mafuta.
 2. Tia nyanya zilizosagwa pamoja na nyanya kopo, tia nanaa, kotmiri, chumvi na pilipili.
 3. Kaanga hadi nyanya ziwive na rojo liwe zito iache ipowe.

Kidokezo:

Mikate unaweza kutumia chapatti kavu badala ya Tortillas ikiwa haipatikani.

Masala ikiwa hukupata ya Taco weka masala yoyote upendayo, kama oregano, mdalasini, jira (cumin)

 

 

 

Share