Hirizi (Taveez) Zilizo Na Aayah Na Namba Kwa Ajili Ya Kinga Ni Shirk?

 

SWALI:

Ahsanteni sana kwa majibu yenu ya haraka on my last question. Leo naomba kuuliza is wearing of Taveez valid in Islam? Is there any reference made in Qur’an and, or Hadith in its support? Many people wear Taveez having some Qur’anic verses or some alphabetical or numerical tables, thinking that it will save them from trouble. Is it correct?

Jazakallah kheir

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu mas-ala ya hirizi. Hakika ni kuwa maswali kama haya tumeyajibu mara nyingi lakini hata hivyo hakuna tatizo kulijibu hili mara nyingine tena.

Uislamu umekuja kumpatia mwanadamu uhuru kwa kiasi kikubwa. Katika kumtoa utumwani umemuamuru atake msaada na amuombe Muumba, Allaah Aliyetukuka peke Yake. Kuamini kuwa vipo vitu au vikaratasi ambavyo vinaweza kumsaidia ni kujiingiza katika ushirikina ambao umepigwa vita na Uislamu kwa kiasi kikubwa.

Hivyo hivyo, zipo Hadiyth ambazo zinatuelezea ushirikina na uharamu wa kutundika au kuvaa hirizi kwa nia yoyote ile. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

Mwenye kutungika hirizi, hakika amefanya shirki” (Ahmad).

Na kauli yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

Aliyetungika hirizi basi Allaah Hamtimizii shida yake, na mwenye kutungika azima basi Allaah hamuondolei alichonacho” (al-Haakim).

Na kauli yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pale alipomuona kipofu mmoja ana kitambaa kakifunga mkononi mwake cha njano alimuuliza: “Kwa nini umefanya hivi?” Akasema: “Hii ni kutoka na wahina (tatizo lililonikuta)”. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Ivue kwani Allaah Aliyetukuka Hatakuzidishia isipokuwa matatizo tu na kama utakufa na hicho kitambaa kiko juu yako basi hautafanikiwa milele” (Ibn Maajah).

Tunaona matatizo ya kufanya hayo basi ni juu yetu kujiepusha navyo ili tusiwe ni wenye kupata matatizo hapa duniani na kesho Akhera.

Ingia katika viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Hazina (Hirizi) Inakubalika Au Shirki?

Hirizi Inafaa Kuvaliwa Kutibu Maradhi Ya Nafsi Na Jini?

Na Allaah Anajua zaidi.

 

Share