Skip to main content

Maandazi Ya Kukandiwa Kwa Maziwa

Maandazi Ya Kukandiwa Kwa Maziwa

Vipimo

Unga - 4 vikombe vya chai

Sukari - 1 kikombe cha chai

Hamira - 1 kijiko cha chai

Samli - 1 kijiko cha chai

Maziwa  - 1 ½ kikombe cha chai

Hiliki -  kiasi

Mafuta ya kukaangia -  kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

  1. Changanya unga,  hamira, samli, maziwa, kisha  vuruga na kanda ukandike kiasi.
  2. Kata madonge manane kisha acha uumuke.
  3. Ukishaumuka sukuma kila donge ukate vipande vinne. 
  4. Panga kwenye meza tena yaumuke.
  5. Weka mafuta ya kukaangia katika karai na yakaange kwa moto mkali wa kiasi.
  6. Yatoe weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa.  

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)