Majusa Ni Mtu Gani Katika Kaumu Gani?

 

Majusa Ni Mtu Gani Katika Kaumu Gani?

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Asalamu aleikum ndugu alhidaaya tunafurahi kwa yenu website sababu mengi tunajifunza namengi tuna ulizziyia munatujibu kwa uwezo waallah subhaanahu waa taala; Suali langu kuna kisa nimekiiskia cha umtu anae itwa (Majusa) Huyu Majusa Ni Umtu Gani Nikatika Qomu Gani Tafadhali Munijibu? Sababu Kisa Chenyewe Kinamalizikia Kakuwa Majusa Ameingia Peponi Ok Nimuhimu Kujulishana Kwa Mambo Ya Tarikhi?

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Hatuna uhakika kama umekusudia hilo katika swali lako au kama umekusudia kuuliza kuhusu Juuj na Ma’ajuuj.

 

Ikiwa hivyo ulivyoandika ndivyo ulivyokusudia basi hii ni kaumu ambayo inaitwa Majusi na sio Majusa. Hawa ni watu waliokuwa wakiabudu moto hata kabla ya kuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hii ni kaumu iliyokuwa ikipatikana Uajemi (Fursi au Iran kwa sasa). Na watu hao wenye kuabudu moto wanapatikana hadi sasa katika nchi ya Iran, India na nchi nyinginezo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share