Masiyh Ad-Dajjaal Atafufuliwa Tena Siku Ya Qiyaamah Kufitinisha Watu

Masiyh Ad-Dajjaal Atafufuliwa Tena Siku Ya Qiyaamah Kufitinisha Watu

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Assalaam Alaykum Warahmatul Laahi Wabarakat Ama Baad, Mashehe zetu tunakutakieni kila la kheri na kazi zenu za daawa na Allah akujaalieni pamoja na sote, ama nimesoma kwa urefu makala yenu kuhusu massihi dajaali kwa namna atakavotokea na mpaka kuuliwa kwake. sasa mimi nauliza suala huyu dajaali baada ya kufa atafufuliwa tena siku ya kiaama na kuanza kufitinisha kama alivofanya hapa duniani, ni hayo tu ila majibu yetu mnatuchewesha lakini In Shaa Allah Allaah atakufanyieni wepesi.

 

Maasalaam.

 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Masiyh Ad-Dajjaal ni kiumbe ambaye Ataletwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kabla ya Qiyaamah na atafishwa kabla ya Siku ya Qiyaamah. Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameonya kuhusu kiumbe huyo katika Hadiyth nyingi, miongoni mwazo ni Hadiyth ifuatayo:

 

 

عن ابن عمر رضي الله عنهما، قال: كُنَّا نَتَحَدَّثُ عَنْ حَجَّةِ الوَدَاعِ، والنَّبيُّ صلى الله عليه وسلم بَيْنَ أَظْهُرِنَا، وَلا نَدْرِي مَا حَجَّةُ الوَدَاعِ حَتَّى حَمِدَ اللهَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم وَأثْنَى عَلَيهِ ثُمَّ ذَكَرَ المَسْيحَ الدَّجَّال فَأطْنَبَ في ذِكْرِهِ، وَقَالَ: ((مَا بَعَثَ اللهُ مِنْ نَبيٍّ إلا أنْذَرَهُ أُمَّتَهُ، أنْذَرَهُ نُوحٌ وَالنَّبِيُّونَ مِنْ بَعْدِهِ، وَإِنَّهُ إنْ يَخْرُجْ فِيكُمْ فَما خَفِيَ عَليْكُمْ مِنْ شَأنِه فَلَيْسَ يَخْفَى عَليْكُم، إنَّ رَبَّكُمْ لَيْسَ بأعْوَرَ وإنَّهُ أعْوَرُ عَيْنِ اليُمْنَى، كَأنَّ عَيْنَهُ عِنَبَةٌ طَافِيَةٌ ))  رواه البخاري، وروى مسلم بعضه

Imepokewa kutoka kwa ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa amesema: Tulikuwa tukizungumza Hijjah ya kuaga (Hijjatul Wadaa’) baina yetu wala hatujui nini Hijjah ya kuaga mpaka Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alipomuhimidi Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) na kumtukuza. Baada ya hapo akamtaja Masiyh Dajjaal na kuzungumza kwa kirefu. Kisha akasema: “Kila Rasuli aliyetumwa na Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) amewaonya Ummah wake kuhusu (Masiyh Dajjaal). Nuwh na Rusul waliokuja baada yake walionya kumhusu. Na hakika yeye atatoka miongoni mwenu, hataweza kujificha (kwani tayari mmeshamjua), ukweli wake hautafichika nanyi. Hakika Mola wenu si chogo, bali yeye ni chogo jicho lake kulia kama kwamba jicho lake ni zabibu iliyovimba….   [Al-Bukhaariy na Muslim amepokea baadhi yake)

 

 

 

Hakika ni kuwa viumbe vyote ambavyo vitaishi hapa duniani wana-Aadam  au majini wamekalifishwa kufuata yaliyo mazuri na kuacha yaliyo mabaya. Mwenye kufuata atapata ufanisi wa duniani na Kesho Aakhirah, na wenye kukengeuka basi watapata adhabu hapa duniani na kubwa zaidi Siku ya Qiyaamah. Kwa hiyo, bila shaka Masiyh atafufuliwa na kuhukumiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

   

Bonyeza kifuatacho upate faida zaidi:

 

Masiyh Dajjaal

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share