Maulidi: Ufafanuzi Wa Khofu Ya Kupotea Qur-aan, Zafa (Zefe) Za Maulidi Si Kwa Ajili Makafiri Waujue Uislamu?

 

Maulidi: Ufafanuzi Wa Khofu Ya Kupotea Qur-aan, Zafa (Zefe) Za

Maulidi Si Kwa Ajili Makafiri Waujue Uislamu?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Asalamu Alykum

Natoa shukurani kupata jibu haraka.Jibu lenyewe limechangia ufafanuzi zaidi.Nadhani hamutachoka kutujibu na Allah atawalipa jaza yake.

Katika hoja ya tisa, mumeeleza Khofu ya kupotea Quran kabisa baada kufa kwa wengi waloihifadhi, mukasema haingetufukia na vizazi vyetu. Hapo pataka ufafanuzi, Imani ya walokuwa na hofu juu ya maneno ya Allaah Nahnu Nazzalna Dhikra………ni ipi na ujuzi wao kujua Ghaib.

 

Mawlid: Ikiwa Qur-aan Imehifadhiwa Vipi Swahaba Walikhofia Kupotea? Maulidi Yana Ubaya Gani?

 

Vilevile, sababu zote mulizozieleza za kuhakikisha Quran haitopotea, hofu hiyo tunayo sasa dhidi ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), Atukanwa, akashifiwa, achorwa kibonzo NK Waisilamu sote ni haki na waajib wetu kutumia mbinu zozote kuhakikisha Ulimwengu mzima unamfahamu Nabiy tueneza Sifa na Sera zake. Tuweke kando tafauti baina ya wapingao na wasopinga Mawlid. Waisilamu sote wa madhehebu yote Twamswalia Nabiy kama tulivyofundishwa lakini baada ya kumswalia wasokuwa waisilamu hawajui sifa na sera zake ndipo wakamkejeli. Watakapo tuona twaandamana tukimsifu watatanabahi na watake kumuelewa. Shukran

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Hakika kuandamana kwetu kwa ajili hiyo mara moja kwa mwaka wakati wa mazazi ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) inaleta utata zaidi kuliko kutatua utata. Na sifa tunazomsifu nazo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) huwa ni kwa lugha isiyoeleweka na raia wa nchi ambazo sisi tunaandamana.

 

Pia huwa kuna maswali chungu mzima kwa wakati huu kutoka kwa wasiokuwa Waislamu wakisema: Nyinyi mnasema hatufai kusherehekea mazazi ya Yesu mbona nyinyi mnasherehekea ya Nabiy wenu? Mnatuambia kuwa tusiwe ni wenye kupiga magoma, mbona nyinyi mnapiga? Je, huu ni uchaji wa Allaah aina gani wa kuwazuilia watu kisha nyie mkafanya?

Tunarudi pale pale kuwa lolote linalozuliwa lazima litavunja na kuharibu Sunnah moja au zaidi na bila shaka hilo litaleta madhara katika Ummah.

 

Ili wasiokuwa Waislamu wawe ni wenye kumuelewa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) sio sisi kufanya zafa bali ni sisi kumuiga katika yote aliyokuja nayo kwetu. Tukiwa tutaishi kama Waislamu kweli basi wasiokuwa Waislamu watataka kutufahamu na hapo tutawaelezea kuhusu Uislamu na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Ama kuhusu mas-ala ya khofu ya kupotea Qur-aan, tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo ambavyo vimefafanua  mas-ala hayo:

 

 

Ufafanuzi Sahihi Wa Maana Ya Bid’ah – Kukusanywa Msahafu Ni Bid’ah?

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share