SWALI:
Assalam Alaykum. Ama baada!! Napenda kufahamu Maimamu wako wangapi? Na je kila imamu ana dhehebu lake? Na je wanapatikana kwa kuteuliwa vipi? Tafadhali ningependa kufahamu? Na imamu yupi ni bora kuliko wote?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu idadi ya Maimaam.
Kabla ya kutazama kuhusu idadi hiyo ya Maimaam ni vyema tujue maana ya neno Imaam. Neno Imaam lina maana nyingi kilugha na hata kishari’ah. Imaam ina maana ya kiongozi wa juu katika dola. Pia ina maana ya kiongozi wa Waislamu katika Swalah za jama’ah au pia mjuzi na aliyebobea katika mas-ala ya Dini ya Kiislamu mpaka akaonekana ni msingi wa Waislamu wa kawaida wa kuifahamu Dini
Huenda muulizaji amekusudia maana ya mwisho katika swali
1) ‘Abdur-Rahmaan bin al-Awzaa‘iy, maarufu akijulikana
2) Al-Layth bin Sa‘d, maarufu kwa jina la Imaam al-Layth.
3) Imaam Sufyaan ath-Thawriy.
4) Daawuud bin ‘Aliy, maarufu kwa jina Imaam Daawuud adhw-Dhwaahiriy.
5) Muhammad bin Jariyr bin Yaziyd atw-Twabariy, maarufu kwa Imaam atw-Twaabariy.
6) Imaam Ibn Abi Laylaa.
7) Imaam Abu Thawr.
8) Imaam Ibn Taymiyyah au maarufu kwa Shaykhul Islaam, na wengine wengi.
Jambo muhimu ambalo tunafaa tulijue ni kuwa hawa wanachuoni hawakujitangaza kuwa wao ndio wanaojua kila kitu kwa hivyo Waislamu wawafuate kwa kila jambo.
Hebu tupate mfano wa kauli za Maimaam kuhusu kufuata mambo walioyo yasema kimbumbumbu.
1) Imaam Abu Haniyfah alitoa kauli nzito na za nguvu kuhusu kufuata kiupofu (Taqliyd) rai zake na zile za wanafunzi wake. Alikataza kwa msisitizo mtu yeyote kufuata rai zao au kutoa hukumu za kishari’ah kutegemea kwazo ila tu mtu huyo awe anaelewa zile dalili ambazo yeye na wanafunzi wake wamezitumia na yale machimbuko ambayo wamefikia hitimisho kwa uamuzi huo. Imaam amenukuliwa na mwanafunzi wake, Zufar kuwa alisema, “Haifai kwa yeyote yule asiyejua dalili na hoja zangu kutoa hukumu kulingana na kauli zangu, kwa hakika sisi ni binaadamu na tunaweza kusema kitu leo na kukikataa kesho”.
2) Ibn ‘Abdil-Barr ameripoti kuwa Maalik wakati mmoja alisema, “Hakika ni kuwa mimi ni mwanaadamu, ninakosea na wakati mwengine ninasibu; hivyo chunguzeni vilivyo rai zangu, kisha chukueni yale yanayokubaliana na Kitabu na Sunnah, na yakataeni yote yanayopingana navyo”. Kauli hii ni dalili ya dhahiri kuwa Qur-aan na Hadiyth vilipewa kipaumbele juu ya vitu vyengine vyovyote na mwanachuoni huyu mkubwa ambaye hakuwa na Niyah ya kuwa rai zake zifuatwe pasi na kuchunguzwa.
3) Imaam ash-Shaafi‘iy alitilia mkazo
4) Imaam Ahmad bin Hanbal naye amesema: “Msifuate rai yangu, wala msifuate rai ya Maalik, au Ash-Shaafi'iy au ya Awzaa’iy, wala Ath-Thawriy, lakini chukueni kutoka kule walikotoa"
Katika usimulizi mmoja: "Msiige dini yenu kutoka kwa mtu yeyote katika hawa, bali chochote kilichotoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake, chukueni, kisha kwa At-Taabi'iyn (Waliofuata) ambako mtu ana khiari".
Akaeleza pengine: "Rai ya Awzaaiy, rai ya Maalik, rai ya Abu Haniyfah, zote ni rai, na ni sawa katika macho yangu. Lakini, dalili ni yale masimulizi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake"
Akasema: "Yeyote atakayekanusha kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) basi yumo katika ukingo wa kuangamia"
Na Allaah Anajua zaidi