Faida Za Kusilimu; Kuingia Katika Dini Ya Kiislamu

 

Faida Za Kusilimu; Kuingia Katika Dini Ya Kiislamu

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Ningependa kufahamu faida zote za mtu kuslim (kubadili dini na kuwa muislamu).

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Faida za kusilimu na kuingia katika Dini ya Kiislamu hazielezeki kutokana na wingi wake kama zinavyopatikana katika Qur-aan na Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Kwa kifupi, Uislamu ndio mafanikio ya mwana Aadam ya duniani na Aakhirah. Na mafanikio ya Aakhirah ndio ya muhimu zaidi kwa sababu ndio uhai wa kudumu milele. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾

Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika. [Aal-‘Imraan: 85]

 

Dini zote nyinginezo zinamshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na  hivyo hatima yao ni motoni isipokuwa tu ikiwa wafuasi wake watarudi kusilimu katika Dini ya kweli Aliyoichagua Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa waja Wake. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ ﴿١١﴾وَأُمِرْتُ لِأَنْ أَكُونَ أَوَّلَ الْمُسْلِمِينَ ﴿١٢﴾قُلْ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿١٣﴾قُلِ اللَّـهَ أَعْبُدُ مُخْلِصًا لَّهُ دِينِي ﴿١٤﴾فَاعْبُدُوا مَا شِئْتُم مِّن دُونِهِ ۗ قُلْ إِنَّ الْخَاسِرِينَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ أَلَا ذَٰلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ ﴿١٥﴾ لَهُم مِّن فَوْقِهِمْ ظُلَلٌ مِّنَ النَّارِ وَمِن تَحْتِهِمْ ظُلَلٌ ۚ ذَٰلِكَ يُخَوِّفُ اللَّـهُ بِهِ عِبَادَهُ ۚ يَا عِبَادِ فَاتَّقُونِ ﴿١٦﴾وَالَّذِينَ اجْتَنَبُوا الطَّاغُوتَ أَن يَعْبُدُوهَا وَأَنَابُوا إِلَى اللَّـهِ لَهُمُ الْبُشْرَىٰ ۚ فَبَشِّرْ عِبَادِ ﴿١٧﴾الَّذِينَ يَسْتَمِعُونَ الْقَوْلَ فَيَتَّبِعُونَ أَحْسَنَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ هَدَاهُمُ اللَّـهُ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمْ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿١٨﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Hakika mimi nimeamrishwa nimwabudu Allaah nikiwa mwenye kumtakasia Dini Yeye. “Na nimeamrishwa kuwa niwe wa kwanza wa Waislamu.”  Sema: “Hakika nikimuasi Rabb wangu, nina khofu adhabu ya Siku adhimu.”Sema: “Allaah Pekee namwambudu nikimtakasia Yeye tu Dini yangu. “Basi abuduni mnayotaka badala Yake.” Sema: “Hakika waliokhasirika ni wale waliokhasiri nafsi zao na ahli zao Siku ya Qiyaamah. Tanabahi!  Hiyo ndio khasara bayana.”Watapata kutoka juu yao vifuniko vya moto, na chini yao vifuniko. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokhofisha waja Wake. Enyi waja Wangu basi Nikhofuni. Na wale waliojitenga kuabudu taghuti wakarejea kutubia kwa Allaah, watapata bishara njema. Basi wabashirie waja Wangu. Wale wanaosikiliza kwa makini kauli, wakafuata yaliyo mazuri yake zaidi, hao ndio wale Aliowaongoa Allaah, na hao ndio wenye akili. [Az-Zumar: 11- 18]

 

Linalokupasa ili uongoke na uepukane na hatima mbaya ya ukafiri ni kutafuta  elimu Sahihi ya Dini hii tukufu ya Uislamu.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share