Vitabu Vipi Muhimu Vya ‘Aqiydah Tawhiyd Na Fiqh?

 

Vitabu Vipi Muhimu Vya ‘Aqiydah  Tawhiyd Na Fiqh? 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

As salaam alaykum
Nilikua ninaomba ufafanuzi juu ya masuala haya matatu aqidah, tawheed na fiqh. Na je nitumie vitabu vipi ili niweze kustafidi ikiwa mimi ni mchanga kabisa katika dini

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

Wa 'alaykumussalaam wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh

 

Tunashukuru kwa himma yako ya kutafuta uhakika wa baadhi ya mas-alah ya Dini, na hilo ni jambo muhimu.

Kuhusu vitabu vya 'Aqiydah na Tawhiyd, Mwanachuoni mkubwa, Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) kaishafafanua vitabu muhimu vya kusoma katika masomo hayo, soma Fatwa ifuatayo hapa chini:
 

 

Imaam Ibn Baaz - Vitabu Bora Kuhusu ‘Aqiydah

Ama kuhusu kitabu cha Fiqh, kuna vitabu kadhaa Wanachuoni wamevipendekeza kuvisoma, kama vile:
 

1. Al-Mulakhasw Al-Fiqhiy cha Shaykh Swaalih bin Fawzaan (Hafidhwahu Allaah).

 

المُلخَّصُ الفِقهيُّ للشَّيخِ الدُّكتور صالحِ بنِ فوزانَ الفوزان
 

2. Aadaab Al-Mashyi ilaa’sw-Swalaah cha Shaykh Al-Islaam Muhammad bin ‘Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah). 

 

آداب المشي إلى الصلاة تأليف: الشيخ محمد بن عبد الوهاب رحمه الله تعالى
 

3. Manhajus-Saalikiyn Wa Tawdhwiyhul-Fiqh Fiyd-Diyn  cha Imaam 'Abdur-Rahmaan bin Naaswir As-Sa'diy (Rahimahu Allaah).

 

 منهج السالكين وتوضيح الفقه في الدين، للشيخ عبد الرحمن بن ناصر السعدي - رحمه الله 
 

Kadhalika vitabu hivi vifuatavyo vya Ahaadiyth, vimekusanya masuala ya Fiqh kwa uzuri:
 

 
4. 'Umdatu Al-Ahkaam cha 'Abdul-Ghaniy Al-Maqdisiy (Rahimahu Allaah). 

 

 عمدة الأحكام في كلام خير الأنام  الحافظ عبد الغني المقدسي
 

5. Buluwgh Al-Maraam cha Ibn Hajar Al-Asqalaaniy (Rahimahu Allaah).

 

 بلوغ المرام من أدلة الأحكام: أحمد بن علي بن حجر العسقلاني

 

Hiki tumeanza kukifasiri kinapatikana hapa:

 

 

http://www.alhidaaya.com/sw/sunnah_hadiyth

 

 

Vilevile utavipata baadhi ya vitabu vya Tawhiyd ndani ya www.alhidaaya.com, ingia katika kiungo hapa chini:
 

http://www.alhidaaya.com/sw/vitabu 

Wa Allaahu A'lam

 

 

Share