Nimemuoa Mwanamke Mbudhi (Budhist), Je Nimuache?

SWALI:

 

Asaalam Alekum Warhamutulah Taala Wabarakatu, natowa shukrani zangu kwa waisilam wa ALHIDAAYA.   Swali langu ni kuhusu ndoa nimeowa mke Budist kutokana na uchache wa elimu ya dini yetu na nimeowa kwa shari’ah ya kidini na nimesoma si ruhusa kuowa Budist mpaka aamini na mke mpaka sasa hajabadili dini je nimuche? Au nifanye nini?

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kumuoa mwanamke ambaye ni Mbudhi.

Hakika kama ulivyosema ndivyo Allaah Aliyetukuka Anavyotuambia:

Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni” (al-Baqarah [2]: 221).

Kwa hiyo, huna budi isipokuwa umuache na utafute mwengine kwani mwanzo hakuna ndoa kishari’ah baina yako na yeye.

Isitoshe ndugu yetu, tusiwe na tabia ya kufanya mambo ambayo hatuyajui au hatuna uhakika nayo kasha ndio tunakuja kuuliza. Kufanya hivyo kutapelekea katika madhambi kwani ulikuwa unaweza kuuliza tokea mwanzo na hukufanya. Hii ni tabia waliyonayo Waislam wengi hivi sasa; hujiingiza kwenye matatizo, haraam, utata na kasha baadaye ndio wanauliza hukmu ya kishari’ah. Tusiwe hivyo Waislam na tumuogope Allaah katika mambo yetu yote.

Bonyeza kiungo kifutacho upate manufaa zaidi:

Ameoa Mwanamke Mshirikina Na Hataki Hadi Sasa Kubadili Dini Yake Nini Hukmu Ya Ndoa Yake? 

Anaweza Kufunga Ndoa Na Mwanaume Mshirikina Bila Ya Kitendo Cha Ndoa Hadi Asilimu? Hapati Waume Wa Kiislamu Naye Anataka Sitara

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share