Mama Mshirikina Anataka Twende Kwake Baada ya Kuaga Dunia Baba Yetu

SWALI:

 

Asalam aleykum,

 
nashukuru kwa majibu yenu. ila nina swali linalonisumbuwa sana.
Kwa kweli ni mtihani, katika familiya yetu tumezaliwa 9. kwa mama yangu tuko 6, na kwa mama wa pili ni 3.waliachana toka mwaka 2007, kwa matatizo tu, na kukosa kuwaminiana  tukaendelea kuishi na baba yetu mzazi akaowa, mwaka 2007/10 baba yetu akaaga dunia, tukabaki na mama yetu wa kufikia na wote tukamuwa tuake wote pamoja mama mzazi wetu toka wachane alirudi kwao.  Alivyo fariki baba mama akataka watoto wake twende tukakae naye, kwa mama tupo wasichana wa nne, wa vulana wawili
moja wa kike ameolewa, yuko kwake kwa mumewe. ila tuliyobaki wote tuko pamoja. wa kiume aliyo kuwa mkubwa ndiyo msimamizi wa familiya.
 
Tatizo ni kwamba mama na baba waliwahi kugombana kwa ajili ya mali kati yao.na pia mama alikuwa anatabiya ya shirki.  Swali langu ni, mama yangu anataka tuwende tukakai naye tuwache hawa mayatima yani wadogo zetu na mamayao peke yao.  na ukitazama hawa ngugu yoyote karibu.  Kaka yangu akamuliza mama je uanuhakika gani kama utaishi maisha mile hapa duniani?  Hana la kujibu, kwakweli ni mtihani sasa analolifanya ni shirki na mpaka sasa hivi anatuma jini na mambo kibao, inavyosemekana kwamba anaagizisha majinina ndiyo kazi yake. 

 
swali langu ni hivi tkimlea na kumti ila awe mbali na sisi kwa sababu tukikanaye atatufarakisha hata sijui tufanyeje kwa kweli tunataka dua ya ke ila ni mtiha  tafhadhali kwania ba ya ndugu zangu wote naomba utujibu swali hii tufanyeje?


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu mtihani uliowasibu nyie kama ndugu.

Hakika ni kuwa katika swali hilo huna haja ya kubabaika wala kujitia wasiwasi wa bure ambao hautawafaidisha kwa chochote. Nyie vijana wakubwa mna wajibu wa kuwatazama wadogo zenu na kumtazama mama yenu kwa hali na mali.

 

Hata hivyo, ikiwa kweli mama ni mshirikina nyinyi hamfai kumtii katika ushirikina wake na maovu yake lakini mnatakiwa muishi naye kwa wema. Allaah Aliyetukuka Anasema:

Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii. Lakini kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anayeelekea Kwangu. Kisha marejeo yenu ni Kwangu Mimi, na Mimi nitakuambieni mliyokuwa mkiyatenda” (Luqmaan [31]: 15).

 

Kwa hivyo, nasaha yetu kwenu ni nyinyi mkae mlipo lakini mtazameni mama yenu kwa kila njia ambayo mnaweza na Allaah Aliyetukuka Atawakinga na shari zake ikiwa kweli mnayoyasema ni kweli.

 

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Wazazi Wangu Wako Kwenye Maasi,Ushirikina Wa Waganga Na Albadiri (Ahlul-Badr)

 

 

Inafaa Kukata Undugu Na Dada Anayefanya Ushirikina Na Kupenda Starehe Za Dunia?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share