Achari Tamu Na Kali Ya Karoti Na Nyanya/Tungule

Achari Tamu Na Kali Ya Karoti Na Nyanya/Tungule

Vipimo

Karoti - 5

Nyanya/tungule - 7

Kitunguu maji - 3

Pilipili mbichi - 3

Nyanya kopo (tomato paste) - 2 vijiko vya supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7 chembe

Pilipili ya unga nyekundu - 2 vijiko vya supu

Mafuta - ¼ kikombe

Sukari - 2 vijiko vya supu

Ndimu - 3

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katakata vitunguu, nyanya, weka kando
  2. Kuna/puruza (grate) au katakata kitunguu thomu vidogodogo  weka kando
  3. Katakata pilipili mbichi vipande virefu virefu weka kando
  4. Safisha karoti  kisha katakata vipande virefuvirefu vya kiasi weka kando.
  5. Weka mafuta katika karai, kisha tia, kitunguu maji na cha thomu, nyanya, pilipili mbichi na ya unga, nyanya kopo (paste), chumvi. Vichanganye pamoja kabla ya kuweka katika moto.
  6. Weka katika moto mdogo, funika uive mchanganyiko. Usikoroge. Karibu na kukaanza kukauka tia karoti, sukari  na ndimu, kisha ndio ukoroge kidogo kuchanganya.
  7. Acha katika moto kwa dakika moja tu ili karoti zisiive na kulainika, bali  zibakie kuwa ngumu.
  8. Onja chumvi na ongeza pilipili na ndimu ukipenda iwe kali zaidi.   Tayari kuliwa na chakula chochote upendacho.  
Share