021 - Al-Anbiyaa

 

  الأنْبِيآء

 

021-Al-Anbiyaa

 

021-Al-Anbiyaa: Utangulizi Wa Suwrah

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

اقْتَرَبَ لِلنَّاسِ حِسَابُهُمْ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ مُّعْرِضُونَ ﴿١﴾

1. Imewakaribia watu hesabu yao, nao wamo katika mghafala wanakengeuka (na wanapuuza).

 

 

 

مَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّن رَّبِّهِم مُّحْدَثٍ إِلَّا اسْتَمَعُوهُ وَهُمْ يَلْعَبُونَ ﴿٢﴾

2. Hauwafikii Ukumbusho wowote ule mpya kutoka kwa Rabb wao isipokuwa huusikiliza kwa makini na huku wao wanacheza.

 

 

 

لَاهِيَةً قُلُوبُهُمْ ۗ وَأَسَرُّوا النَّجْوَى الَّذِينَ ظَلَمُوا هَلْ هَـٰذَا إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ ۖ أَفَتَأْتُونَ السِّحْرَ وَأَنتُمْ تُبْصِرُونَ ﴿٣﴾

3. Huku nyoyo zao zimeghafilika. Na wale waliodhulumu hunong’onezana kwa siri:  Je, ni nani huyu isipokuwa ni binaadam kama nyinyi? Je, mnaiendea sihiri hii na hali nyinyi mnaona?  

 

 

 

قَالَ رَبِّي يَعْلَمُ الْقَوْلَ فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٤﴾

4. (Nabiy Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Rabb wangu Anajua yasemwayo katika mbingu na ardhi, Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

بَلْ قَالُوا أَضْغَاثُ أَحْلَامٍ بَلِ افْتَرَاهُ بَلْ هُوَ شَاعِرٌ فَلْيَأْتِنَا بِآيَةٍ كَمَا أُرْسِلَ الْأَوَّلُونَ ﴿٥﴾

5.   Lakini wakasema: (Qur-aan) Ni ndoto za mkorogano! Bali ameitunga! Bali yeye ni mshairi![1] Basi atuletee Aayah (Muujiza) kama walivyotumwa wa awali.

 

 

 

مَا آمَنَتْ قَبْلَهُم مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا ۖ أَفَهُمْ يُؤْمِنُونَ ﴿٦﴾

6. Hawakuamini kabla yao (umati wa) mji wowote Tuliouangamiza. Je, basi wao wataamini?

 

 

 

وَمَا أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِمْ ۖ فَاسْأَلُوا أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٧﴾

7. Na Hatukutuma kabla yako isipokuwa wanaume Tunawafunulia Wahy. Basi waulizeni wajuzi (wa Taurati na Injiyl) mkiwa hamjui.

 

 

 

وَمَا جَعَلْنَاهُمْ جَسَدًا لَّا يَأْكُلُونَ الطَّعَامَ وَمَا كَانُوا خَالِدِينَ ﴿٨﴾

8. Na Hatukuwafanya (hao Rusuli) kuwa na miili isiyokula chakula, na hawakuwa wenye kudumu.

 

 

ثُمَّ صَدَقْنَاهُمُ الْوَعْدَ فَأَنجَيْنَاهُمْ وَمَن نَّشَاءُ وَأَهْلَكْنَا الْمُسْرِفِينَ ﴿٩﴾

9. Kisha Tukawasadikishia ahadi, Tukawaokoa wao na wale Tuliowataka, na Tukaangamiza wapindukiaji mipaka.

 

 

لَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ كِتَابًا فِيهِ ذِكْرُكُمْ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿١٠﴾

10. Kwa yakini Tumekuteremshieni Kitabu (Qur-aan) ambacho ndani yake mna makumbusho kwenu. Je, basi hamtii akilini?

 

 

 

وَكَمْ قَصَمْنَا مِن قَرْيَةٍ كَانَتْ ظَالِمَةً وَأَنشَأْنَا بَعْدَهَا قَوْمًا آخَرِينَ ﴿١١﴾

11. Ni miji mingi sana Tumeiteketeza iliyokuwa ikidhulumu, na Tukaanzisha baada yake kaumu nyinginezo.

 

 

 

فَلَمَّا أَحَسُّوا بَأْسَنَا إِذَا هُم مِّنْهَا يَرْكُضُونَ ﴿١٢﴾

12. Basi walipohisi Adhabu Yetu, mara wao wakajaribu kuikimbia.

 

 

 

لَا تَرْكُضُوا وَارْجِعُوا إِلَىٰ مَا أُتْرِفْتُمْ فِيهِ وَمَسَاكِنِكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْأَلُونَ ﴿١٣﴾

13. (Waliambiwa) msikimbie! Na rejeeni kwenye yale mliyoneemeshwa na kuyastarehea, na kwenye maskani zenu ili mpate kuulizwa.

 

 

 

قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿١٤﴾

14. Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa madhalimu.

 

 

 

فَمَا زَالَت تِّلْكَ دَعْوَاهُمْ حَتَّىٰ جَعَلْنَاهُمْ حَصِيدًا خَامِدِينَ ﴿١٥﴾

15. Basi ukaendelea huo kuwa ni wito wao mpaka Tukawafanya waliofyekwa wamezimika.

 

 

 

وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاءَ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ ﴿١٦﴾

16. Na Hatukuumba mbingu na ardhi na yaliyo baina yake kwa mchezo.

 

 

 

لَوْ أَرَدْنَا أَن نَّتَّخِذَ لَهْوًا لَّاتَّخَذْنَاهُ مِن لَّدُنَّا إِن كُنَّا فَاعِلِينَ ﴿١٧﴾

17. Lau Tungelitaka kufanya pumbao, basi Tungejifanyia Sisi Wenyewe, lau kama Tungelikuwa Wafanyaji (pumbao). 

 

 

 

بَلْ نَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَى الْبَاطِلِ فَيَدْمَغُهُ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ ۚ وَلَكُمُ الْوَيْلُ مِمَّا تَصِفُونَ ﴿١٨﴾

18. Bali Tunavurumisha haki dhidi ya batili ikaitengua, na mara hiyo inatoweka. Na ole wenu kutokana na mnayoyavumisha.

 

 

 

وَلَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَنْ عِندَهُ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَلَا يَسْتَحْسِرُونَ ﴿١٩﴾

19. Na ni Wake wote waliomo katika mbingu na ardhi. Na (Malaika) ambao wako Kwake hawatakabari wakaacha kumwabudu, na wala hawachoki.

 

 

 

يُسَبِّحُونَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لَا يَفْتُرُونَ ﴿٢٠﴾

20. Wanasabihi usiku na mchana, hawaishiwi nguvu.

 

 

 

أَمِ اتَّخَذُوا آلِهَةً مِّنَ الْأَرْضِ هُمْ يُنشِرُونَ ﴿٢١﴾

21. Je, wamechukua waabudiwa katika ardhi wanaofufua?

 

 

 

لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللَّـهُ لَفَسَدَتَا ۚ فَسُبْحَانَ اللَّـهِ رَبِّ الْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿٢٢﴾

22.  Lau wangelikuweko humo (mbinguni na ardhini) waabudiwa badala ya Allaah, bila shaka zingelifisidika. Basi Subhaana Allaah! Utakasifu ni wa Allaah Rabb wa ‘Arsh kutokana na ambayo wanavumisha.[2]

 

 

 

لَا يُسْأَلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْأَلُونَ ﴿٢٣﴾

23. Haulizwi (Allaah) kwa yale Anayoyafanya, lakini wao wataulizwa.

 

 

 

أَمِ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ آلِهَةً ۖ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ ۖ هَـٰذَا ذِكْرُ مَن مَّعِيَ وَذِكْرُ مَن قَبْلِي ۗ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ الْحَقَّ ۖ فَهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٢٤﴾

24. Je, wamejichukulia badala Yake waabudiwa? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآلهوسلم): Leteni burhani yenu. Hii (Qur-aan) ni ukumbusho wa walio pamoja nami, na ni ukumbusho wa walio kabla yangu, bali wengi wao hawajui haki, na kwa hivyo wao ni wenye kukengeuka.

 

 

 

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ ﴿٢٥﴾

25. Na Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Rasuli yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: Hakika hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, basi Niabuduni.[3]

 

 

 

وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۚ بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ ﴿٢٦﴾

26. Na wakasema: Ar-Rahmaan Amejifanyia mwana! Subhaanah! (Utakasifu ni Wake!) Bali (hao) ni waja waliokirimiwa.[4]

 

 

 

لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ ﴿٢٧﴾

27. Hawamtangulii (Allaah) kwa kauli, nao kwa Amri Yake wanatenda.

 

 

 

يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِ مُشْفِقُونَ ﴿٢٨﴾

28. Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao, na wala hawataomba shafaa’ah (uombezi wowote) isipokuwa kwa yule ambaye (Allaah) Amemridhia[5], nao kutokana na kumkhofu, ni wenye khofu na kutahadhari.

 

 

 

وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّي إِلَـٰهٌ مِّن دُونِهِ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ ﴿٢٩﴾

29. Na yeyote yule miongoni mwao atakayesema: Mimi ni mwabudiwa badala Yake, basi huyo Tutamlipa Jahannam. Hivyo ndivyo Tunavyolipa madhalimu.

 

 

 

أَوَلَمْ يَرَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ كَانَتَا رَتْقًا فَفَتَقْنَاهُمَا ۖ وَجَعَلْنَا مِنَ الْمَاءِ كُلَّ شَيْءٍ حَيٍّ ۖ أَفَلَا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٠﴾

30. Je, hawakuona wale waliokufuru kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeshikamana Tukazibabandua?   Na Tukajaalia kutokana na maji kila kitu kilicho hai?   Je, basi hawaamini?[6]

 

 

 

وَجَعَلْنَا فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِهِمْ وَجَعَلْنَا فِيهَا فِجَاجًا سُبُلًا لَّعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ ﴿٣١﴾

31. Na Tukajaalia katika ardhi milima thabiti isiwayumbie yumbie, na Tukajaalia humo njia pana za kupitika ili wapate kujua waendako.

 

 

 

وَجَعَلْنَا السَّمَاءَ سَقْفًا مَّحْفُوظًا ۖ وَهُمْ عَنْ آيَاتِهَا مُعْرِضُونَ ﴿٣٢﴾

32. Na Tukajaalia mbingu kuwa ni paa lililohifadhiwa. Lakini wao wanazipuuzilia mbali Aayaat (Ishara, Dalili) zake.

 

 

وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ ﴿٣٣﴾

33. Naye Ndiye Ambaye Ameumba usiku na mchana, na jua na mwezi.  Vyote vinaogelea katika falaki.[7]   

 

 

 

وَمَا جَعَلْنَا لِبَشَرٍ مِّن قَبْلِكَ الْخُلْدَ ۖ أَفَإِن مِّتَّ فَهُمُ الْخَالِدُونَ ﴿٣٤﴾

34. Na Hatukujaalia kwa mtu yeyote kabla yako kuwa ni mwenye kudumu. Je, kwani ukifa basi wao watadumu?

 

 

 

كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَنَبْلُوكُم بِالشَّرِّ وَالْخَيْرِ فِتْنَةً ۖ وَإِلَيْنَا تُرْجَعُونَ ﴿٣٥﴾

35. Kila nafsi itaonja mauti.  Na Tutakujaribuni kwa mitihani ya shari na kheri. Na Kwetu mtarejeshwa.

 

 

 

وَإِذَا رَآكَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَـٰذَا الَّذِي يَذْكُرُ آلِهَتَكُمْ وَهُم بِذِكْرِ الرَّحْمَـٰنِ هُمْ كَافِرُونَ ﴿٣٦﴾

36. Na wanapokuona wale waliokufuru hawakufanyi wewe isipokuwa kichekesho tu. (Wakisema): Je, si ndiye huyu anayewataja (vibaya) waabudiwa wenu? Na hali wao ni wenye kukufuru kwa kutajwa Ar-Rahmaan.[8]

 

 

 

خُلِقَ الْإِنسَانُ مِنْ عَجَلٍ ۚ سَأُرِيكُمْ آيَاتِي فَلَا تَسْتَعْجِلُونِ ﴿٣٧﴾

37. Binaadam ameumbwa kuwa na pupa. Nitakuonyesheni Aayaat (Adhabu, Kisasi, Hukmu) Zangu, basi msiniharakize.

 

 

 

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٣٨﴾

38. Na wanasema: Lini itakuwa hiyo ahadi (ya kuadhibiwa)[9] mkiwa ni wakweli? 

 

 

 

لَوْ يَعْلَمُ الَّذِينَ كَفَرُوا حِينَ لَا يَكُفُّونَ عَن وُجُوهِهِمُ النَّارَ وَلَا عَن ظُهُورِهِمْ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ﴿٣٩﴾

39. Lau wangelijua wale waliokufuru wakati pale ambapo hawatoweza kukinga nyuso zao na moto, na wala migongo yao, na wala wao hawatonusuriwa. 

 

 

 

بَلْ تَأْتِيهِم بَغْتَةً فَتَبْهَتُهُمْ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ رَدَّهَا وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿٤٠﴾

40. Bali utawafikia ghafla, uwashtue wapigwe na butwaa, kisha hawatoweza kuurudisha, na wala wao hawatopewa muhula.

 

 

 

وَلَقَدِ اسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِالَّذِينَ سَخِرُوا مِنْهُم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ ﴿٤١﴾

41. Na walikwishafanyiwa istihzai Rusuli kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Kwa hiyo wale waliowafanyia   dhihaka, iliwafikia (adhabu) kwa sababu ya waliyokuwa wakiyafanyia istihzai.

 

 

 

قُلْ مَن يَكْلَؤُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ مِنَ الرَّحْمَـٰنِ ۗ بَلْ هُمْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِم مُّعْرِضُونَ ﴿٤٢﴾

42. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nani awezaye kukulindeni na kukuhifadhini usiku na mchana kutokana na (adhabu ya) Ar-Rahmaan? Bali wao ni wenye kupuuzilia mbali Ukumbusho wa Rabb wao.

 

 

 

أَمْ لَهُمْ آلِهَةٌ تَمْنَعُهُم مِّن دُونِنَا ۚ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَ أَنفُسِهِمْ وَلَا هُم مِّنَّا يُصْحَبُونَ ﴿٤٣﴾

43. Je, kwani wana waabudiwa wanaoweza kuwakinga Nasi? Hawawezi kujinusuru nafsi zao na wala hawatolindwa Nasi.

 

 

 

بَلْ مَتَّعْنَا هَـٰؤُلَاءِ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ طَالَ عَلَيْهِمُ الْعُمُرُ ۗ أَفَلَا يَرَوْنَ أَنَّا نَأْتِي الْأَرْضَ نَنقُصُهَا مِنْ أَطْرَافِهَا ۚ أَفَهُمُ الْغَالِبُونَ ﴿٤٤﴾

44. Bali Tuliwastarehesha hawa (makafiri) na baba zao mpaka ukatawilika umri kwao. Je, hawaoni kwamba Tunaifikia ardhi hii, Tunaipunguza ncha zake?[10] Je, basi wao watashinda?

 

 

 

قُلْ إِنَّمَا أُنذِرُكُم بِالْوَحْيِ ۚ وَلَا يَسْمَعُ الصُّمُّ الدُّعَاءَ إِذَا مَا يُنذَرُونَ ﴿٤٥﴾

45. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi nakuonyeni kwa Wahy. Lakini viziwi hawasikii wito wanapotahadharishwa.

 

 

 

وَلَئِن مَّسَّتْهُمْ نَفْحَةٌ مِّنْ عَذَابِ رَبِّكَ لَيَقُولُنَّ يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿٤٦﴾

46. Na kama wataguswa na mpapaso mdogo tu wa Adhabu ya Rabb wako, kwa hakika watasema: Ole wetu!  Hakika sisi tulikuwa madhalimu.

 

 

 

وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا ۖ وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا ۗ وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ ﴿٤٧﴾

47. Na Tutaweka mizani za uadilifu Siku ya Qiyaamah. Basi nafsi haitodhulumiwa kitu chochote. Na japo ikiwa (amali ina) uzito wa punje ya haradali,[11] Tutaileta. Nasi Tunatosha Kuwa Wadhibiti hesabu.

 

 

 

وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَىٰ وَهَارُونَ الْفُرْقَانَ وَضِيَاءً وَذِكْرًا لِّلْمُتَّقِينَ ﴿٤٨﴾

48. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa na Haaruwn pambanuo (la haki na batili), na mwanga, na ukumbusho kwa wenye taqwa.

 

 

 

الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِالْغَيْبِ وَهُم مِّنَ السَّاعَةِ مُشْفِقُونَ ﴿٤٩﴾

49. Wale wanaomkhofu Rabb wao wakiwa mbali na macho ya watu, nao wanaikhofu Saa.

 

 

 

وَهَـٰذَا ذِكْرٌ مُّبَارَكٌ أَنزَلْنَاهُ ۚ أَفَأَنتُمْ لَهُ مُنكِرُونَ ﴿٥٠﴾

50. Na huu ni ukumbusho wenye baraka (Qur-aan), Tumeuteremsha. Je, basi nyinyi mtaukanusha?

 

 

 

وَلَقَدْ آتَيْنَا إِبْرَاهِيمَ رُشْدَهُ مِن قَبْلُ وَكُنَّا بِهِ عَالِمِينَ ﴿٥١﴾

51. Na kwa yakini Tulimpa Ibraahiym uongofu wake kabla, na Tulikuwa Wenye kumjua vizuri.

 

 

 

إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَا هَـٰذِهِ التَّمَاثِيلُ الَّتِي أَنتُمْ لَهَا عَاكِفُونَ ﴿٥٢﴾

52. Alipomwambia baba yake na watu wake: Nini haya masanamu ambayo nyinyi mnayakalia kuyaabudu?

 

 

 

قَالُوا وَجَدْنَا آبَاءَنَا لَهَا عَابِدِينَ ﴿٥٣﴾

53. Wakasema: Tumewakuta baba zetu wakiyaabudu.

 

 

 

قَالَ لَقَدْ كُنتُمْ أَنتُمْ وَآبَاؤُكُمْ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٥٤﴾

54. Akasema: Kwa yakini mmekuwa nyinyi na baba zenu katika upotofu bayana.

 

 

 

قَالُوا أَجِئْتَنَا بِالْحَقِّ أَمْ أَنتَ مِنَ اللَّاعِبِينَ ﴿٥٥﴾

55. Wakasema: Je, umetujia kwa haki, au wewe ni miongoni mwa wafanyao mchezo?

 

 

 

قَالَ بَل رَّبُّكُمْ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الَّذِي فَطَرَهُنَّ وَأَنَا عَلَىٰ ذَٰلِكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٥٦﴾

56. Akasema: Bali Rabb wenu ni Rabb wa mbingu na ardhi, Ambaye Amezianzisha, nami ni katika wenye kushuhudia hayo. 

 

 

 

وَتَاللَّـهِ لَأَكِيدَنَّ أَصْنَامَكُم بَعْدَ أَن تُوَلُّوا مُدْبِرِينَ ﴿٥٧﴾

57. Na naapa kwa Allaah! Lazima nitafanyia hila masanamu yenu baada ya mkishageuka kwenda zenu. 

 

 

 

فَجَعَلَهُمْ جُذَاذًا إِلَّا كَبِيرًا لَّهُمْ لَعَلَّهُمْ إِلَيْهِ يَرْجِعُونَ ﴿٥٨﴾

58. Basi akayavunja vipande vipande isipokuwa kubwa lao ili wapate kulirejea.

 

 

 

قَالُوا مَن فَعَلَ هَـٰذَا بِآلِهَتِنَا إِنَّهُ لَمِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٥٩﴾

59. Wakasema: Nani amefanya hivi kwa waabudiwa wetu? Hakika yeye ni miongoni mwa madhalimu.

 

 

 

قَالُوا سَمِعْنَا فَتًى يَذْكُرُهُمْ يُقَالُ لَهُ إِبْرَاهِيمُ ﴿٦٠﴾

60. Wakasema: Tulimsikia kijana akiwataja anaitwa Ibraahiym.

 

 

 

قَالُوا فَأْتُوا بِهِ عَلَىٰ أَعْيُنِ النَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَشْهَدُونَ ﴿٦١﴾

61. Wakasema: Mleteni mbele ya macho ya watu ili wapate kushuhudia.

 

 

 

قَالُوا أَأَنتَ فَعَلْتَ هَـٰذَا بِآلِهَتِنَا يَا إِبْرَاهِيمُ ﴿٦٢﴾

62. Wakasema: Je, ni wewe uliyefanya hivi kwa waabudiwa wetu, ee Ibraahiym?

 

 

 

قَالَ بَلْ فَعَلَهُ كَبِيرُهُمْ هَـٰذَا فَاسْأَلُوهُمْ إِن كَانُوا يَنطِقُونَ ﴿٦٣﴾

63. Akasema: Hapana, bali amefanya hayo hili kubwa lao. Hivyo waulizeni wakiwa wanaweza kunena!

 

 

 

فَرَجَعُوا إِلَىٰ أَنفُسِهِمْ فَقَالُوا إِنَّكُمْ أَنتُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٦٤﴾

64. Basi wakajirudia nafsi zao, wakasema: Hakika nyinyi ndio madhalimu.

 

 

 

ثُمَّ نُكِسُوا عَلَىٰ رُءُوسِهِمْ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا هَـٰؤُلَاءِ يَنطِقُونَ ﴿٦٥﴾

65. Kisha wakarudia hali yao ya mwanzo ya upotofu. (Wakasema): Umekwishajua kwamba hawa hawasemi.

 

 

 

قَالَ أَفَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَنفَعُكُمْ شَيْئًا وَلَا يَضُرُّكُمْ ﴿٦٦﴾

66. (Ibraahiym) akasema: Je, basi mnaabudu badala ya Allaah visivyokunufaisheni kitu chochote wala kukudhuruni?

 

 

 

أُفٍّ لَّكُمْ وَلِمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٧﴾

67. Aibu yenu nyinyi na vile mnavyoviabudu badala ya Allaah. Je, hamtii akilini?

 

 

 

قَالُوا حَرِّقُوهُ وَانصُرُوا آلِهَتَكُمْ إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ ﴿٦٨﴾

68. Wakasema: Mchomeni moto na mnusuru waabudiwa wenu, mkiwa ni wafanyao (kunusuru).[12]

 

 

 

قُلْنَا يَا نَارُ كُونِي بَرْدًا وَسَلَامًا عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ ﴿٦٩﴾

69. Tukasema: Ee moto! Kuwa baridi, na salama juu ya Ibraahiym.[13]

 

 

 

وَأَرَادُوا بِهِ كَيْدًا فَجَعَلْنَاهُمُ الْأَخْسَرِينَ ﴿٧٠﴾

70. Na wakamkusudia njama, lakini Tukawafanya wao ndio wenye kukhasirika.

 

 

 

وَنَجَّيْنَاهُ وَلُوطًا إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا لِلْعَالَمِينَ ﴿٧١﴾

71. Na Tukamuokoa yeye pamoja na Luutw kuelekea ardhi (ya Sham) ambayo Tumeibariki humo kwa walimwengu.[14]

 

 

 

وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ نَافِلَةً ۖ وَكُلًّا جَعَلْنَا صَالِحِينَ ﴿٧٢﴾

72. Na Tukamtunukia Is-haaq na (mjukuu) Ya’quwb kuwa ni ziada. Na wote Tumewajaalia kuwa Swalihina.

 

 

 

وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِمْ فِعْلَ الْخَيْرَاتِ وَإِقَامَ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءَ الزَّكَاةِ ۖ وَكَانُوا لَنَا عَابِدِينَ ﴿٧٣﴾

73. Na Tukawafanya Imaam wanaongoza kwa Amri Yetu, na Tukawatia ilhamu kufanya kheri, na kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah. Na wakawa wenye kutuabudu.

 

 

 

وَلُوطًا آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْقَرْيَةِ الَّتِي كَانَت تَّعْمَلُ الْخَبَائِثَ ۗ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمَ سَوْءٍ فَاسِقِينَ ﴿٧٤﴾

74. Na Luutw Tulimpa hikmah na ilimu, na Tukamuokoa kutoka mji ambao ulikuwa unatenda ukhabithi. Hakika wao walikuwa watu waovu, mafasiki.

 

 

 

وَأَدْخَلْنَاهُ فِي رَحْمَتِنَا ۖ إِنَّهُ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٧٥﴾

75. Na Tukamuingiza katika Rehma Yetu. Hakika yeye ni miongoni mwa Swalihina.

 

 

 

وَنُوحًا إِذْ نَادَىٰ مِن قَبْلُ فَاسْتَجَبْنَا لَهُ فَنَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ ﴿٧٦﴾

76. Na Nuwh alipoita hapo zamani.  Tukamuitikia na Tukamuokoa pamoja na ahli zake kutokana na janga kuu.[15]

 

 

 

وَنَصَرْنَاهُ مِنَ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمَ سَوْءٍ فَأَغْرَقْنَاهُمْ أَجْمَعِينَ ﴿٧٧﴾

77. Na Tukamnusuru kutokana na watu ambao walikadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu. Hakika wao walikuwa watu waovu, basi Tuliwagharikisha wote.

 

 

 

وَدَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ إِذْ يَحْكُمَانِ فِي الْحَرْثِ إِذْ نَفَشَتْ فِيهِ غَنَمُ الْقَوْمِ وَكُنَّا لِحُكْمِهِمْ شَاهِدِينَ ﴿٧٨﴾

78. Na Daawuwd na Sulaymaan walipotoa hukmu juu ya konde, walipoingia humo usiku kondoo wa watu wakala mimea, Nasi Tukawa katika hukmu yao hiyo Ni Wenye Kushuhudia.

 

 

 

فَفَهَّمْنَاهَا سُلَيْمَانَ ۚ وَكُلًّا آتَيْنَا حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَسَخَّرْنَا مَعَ دَاوُودَ الْجِبَالَ يُسَبِّحْنَ وَالطَّيْرَ ۚ وَكُنَّا فَاعِلِينَ ﴿٧٩﴾

79. Tukamfahamisha Sulaymaan kadhia hiyo (na hukumu mwafaka). Na kila mmoja Tulimpa hikmah na ilimu. Na Tukatiisha milima iwe pamoja na Daawuwd ikisabihi pamoja na ndege. Na Tukawa Ni Wenye Kufanya (haya).

 

 

 

وَعَلَّمْنَاهُ صَنْعَةَ لَبُوسٍ لَّكُمْ لِتُحْصِنَكُم مِّن بَأْسِكُمْ ۖ فَهَلْ أَنتُمْ شَاكِرُونَ ﴿٨٠﴾

80. Na Tukamfunza (Daawuwd) uundaji wa mavazi ya kivita ya chuma kwa ajili yenu ili yakuhifadhini kutokana na kupigana vita kwenu. Je, basi nyinyi ni wenye kushukuru?

 

 

 

وَلِسُلَيْمَانَ الرِّيحَ عَاصِفَةً تَجْرِي بِأَمْرِهِ إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا ۚ وَكُنَّا بِكُلِّ شَيْءٍ عَالِمِينَ ﴿٨١﴾

81. Na kwa Sulaymaan, (Tulimtiishia) upepo wa dhoruba unaokwenda kwa amri yake katika ardhi ambayo Tumeibariki humo. Nasi Tulikuwa Wenye Kukijua kila kitu.

 

 

 

وَمِنَ الشَّيَاطِينِ مَن يَغُوصُونَ لَهُ وَيَعْمَلُونَ عَمَلًا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ وَكُنَّا لَهُمْ حَافِظِينَ ﴿٨٢﴾

82. Na (Tukamtiishia) miongoni mwa mashaytwaan wakimpigia mbizi na wakimfanyia kazi nyinginezo zisizokuwa hizo. Nasi Tulikuwa Ni Wenye Kuwalinda. 

 

 

 

وَأَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ أَنِّي مَسَّنِيَ الضُّرُّ وَأَنتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿٨٣﴾

83. Na Ayyuwb, alipomwita Rabb wake: Hakika mimi imenigusa dhara, Nawe Ndiye Mbora zaidi wa Kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu.

 

 

 

فَاسْتَجَبْنَا لَهُ فَكَشَفْنَا مَا بِهِ مِن ضُرٍّ ۖ وَآتَيْنَاهُ أَهْلَهُ وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَذِكْرَىٰ لِلْعَابِدِينَ ﴿٨٤﴾

84. Tukamuitikia. Basi Tukamuondoshea dhara aliyokuwa nayo, na Tukampa ahli zake na mfano wao pamoja nao. Ni Rehma kutoka Kwetu, na ni ukumbusho kwa wanaoabudu (Allaah).

 

 

 

وَإِسْمَاعِيلَ وَإِدْرِيسَ وَذَا الْكِفْلِ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّابِرِينَ ﴿٨٥﴾

85. Na Ismaa’iyl na Idriys na Dhul-Kifl[16], wote ni miongoni mwa wenye kusubiri.

 

 

 

وَأَدْخَلْنَاهُمْ فِي رَحْمَتِنَا ۖ إِنَّهُم مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٨٦﴾

86. Na Tukawaingiza katika Rehma Yetu. Hakika wao ni miongoni mwa Swalihina.

 

 

 

وَذَا النُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَاضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ فَنَادَىٰ فِي الظُّلُمَاتِ أَن لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٧﴾

87. Na Dhan-Nuwn (Yuwnus), alipoondoka akiwa ameghadhibika, akadhani kwamba Hatutamdhikisha. Akaita   vizani kwamba: Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Utakasifu ni Wako, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.[17]

 

 

 

فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْغَمِّ ۚ وَكَذَٰلِكَ نُنجِي الْمُؤْمِنِينَ ﴿٨٨﴾

88. Basi Tukamuitikia, na Tukamuokoa kutokana na ghamu. Na hivyo ndivyo Tuwaokowavyo Waumini.

 

 

 

وَزَكَرِيَّا إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ رَبِّ لَا تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ الْوَارِثِينَ ﴿٨٩﴾

89. Na Zakariyyaa, alipomwita Rabb wake: Rabb wangu! Usiniache pekee, Nawe Ndiye Mbora wa wenye kubaki.

 

 

 

فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَوَهَبْنَا لَهُ يَحْيَىٰ وَأَصْلَحْنَا لَهُ زَوْجَهُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ ﴿٩٠﴾

90. Basi Tukamuitikia na Tukamtunukia Yahyaa, na Tukamtengenezea mke wake. Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri na wakituomba kwa raghba na khofu, na walikuwa wenye kutunyenyekea.[18]

 

 

 

وَالَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهَا مِن رُّوحِنَا وَجَعَلْنَاهَا وَابْنَهَا آيَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩١﴾

91. Na (Maryam) ambaye alilinda tupu yake, Tukampulizia (nguoni mwake) katika Ruwh Yetu, na Tukamjaaliya yeye na mwanawe kuwa ni Aayah (Muujiza, Ishara) kwa walimwengu.

 

 

 

إِنَّ هَـٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ ﴿٩٢﴾

92. Hakika huu ummah wenu ni ummah mmoja. Nami ni Rabb wenu, basi niabuduni.

 

 

 

وَتَقَطَّعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ ۖ كُلٌّ إِلَيْنَا رَاجِعُونَ ﴿٩٣﴾

93. Wakafarikiana na kuwa makundi baina yao kuhusu Dini yao. Wote ni wenye kurejea Kwetu.

 

 

 

فَمَن يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَا كُفْرَانَ لِسَعْيِهِ وَإِنَّا لَهُ كَاتِبُونَ ﴿٩٤﴾

94. Basi atakayetenda mema naye ni Muumini, haitakanushwa juhudi yake. Na hakika Sisi Tunamuandikia.

 

 

 

وَحَرَامٌ عَلَىٰ قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا أَنَّهُمْ لَا يَرْجِعُونَ ﴿٩٥﴾

95. Na haiwezekani kwa wanamji wowote ule Tuliouangamiza, kurejea (duniani).  

 

 

 

 

حَتَّىٰ إِذَا فُتِحَتْ يَأْجُوجُ وَمَأْجُوجُ وَهُم مِّن كُلِّ حَدَبٍ يَنسِلُونَ ﴿٩٦﴾

96. Mpaka watakapofunguliwa Yaajuwj na Maajuwj, nao kutoka kila mwinuko watateremka.[19]

 

 

 

وَاقْتَرَبَ الْوَعْدُ الْحَقُّ فَإِذَا هِيَ شَاخِصَةٌ أَبْصَارُ الَّذِينَ كَفَرُوا يَا وَيْلَنَا قَدْ كُنَّا فِي غَفْلَةٍ مِّنْ هَـٰذَا بَلْ كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿٩٧﴾

97. Na itakaribia ahadi ya haki (ya Qiyaamah). Tahamaki macho ya wale waliokufuru yanakodoka (waseme): Ole wetu!  Kwa yakini tulikuwa katika mghafala na haya. Bali tulikuwa madhalimu.

 

 

 

إِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمْ لَهَا وَارِدُونَ ﴿٩٨﴾

98. Hakika nyinyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah ni vichochezi vya moto wa Jahannam, nyinyi mtauingia.[20]

 

 

 

 

لَوْ كَانَ هَـٰؤُلَاءِ آلِهَةً مَّا وَرَدُوهَا ۖ وَكُلٌّ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿٩٩﴾

99. Lau wangelikuwa hawa ni waabudiwa wanaostahiki kuabudiwa basi wasingeliuingia, lakini wote humo ni wenye kudumu.

 

 

 

لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَهُمْ فِيهَا لَا يَسْمَعُونَ ﴿١٠٠﴾

100. Lao kwao humo, ni kupumua kwa mngurumo, nao humo hawatosikia lolote.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ سَبَقَتْ لَهُم مِّنَّا الْحُسْنَىٰ أُولَـٰئِكَ عَنْهَا مُبْعَدُونَ ﴿١٠١﴾

101. Hakika wale ambao imewatangulia Al-Husnaa (furaha, Rehma) kutoka Kwetu, hao watabaidishwa nao (moto).[21]

 

 

لَا يَسْمَعُونَ حَسِيسَهَا ۖ وَهُمْ فِي مَا اشْتَهَتْ أَنفُسُهُمْ خَالِدُونَ ﴿١٠٢﴾

102. Hawatosikia mvumo wake. Nao watadumu katika ambayo zimetamani nafsi zao.

 

 

 

لَا يَحْزُنُهُمُ الْفَزَعُ الْأَكْبَرُ وَتَتَلَقَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ هَـٰذَا يَوْمُكُمُ الَّذِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ ﴿١٠٣﴾

103. Hautowahuzunisha mfazaiko mkubwa kabisa, na Malaika watawapokea (wakiwaambia): Hii ni ile Siku yenu mliyokuwa mkiahidiwa.

 

 

 

يَوْمَ نَطْوِي السَّمَاءَ كَطَيِّ السِّجِلِّ لِلْكُتُبِ ۚ كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُ ۚ وَعْدًا عَلَيْنَا ۚ إِنَّا كُنَّا فَاعِلِينَ ﴿١٠٤﴾

104. Siku Tutakapozikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi zilizoandikwa.[22] Kama Tulivyoanza umbo la awali Tutalirudisha tena.[23] Ni ahadi iliyo juu Yetu. Hakika Sisi Ni Wenye Kufanya

 

 

 

وَلَقَدْ كَتَبْنَا فِي الزَّبُورِ مِن بَعْدِ الذِّكْرِ أَنَّ الْأَرْضَ يَرِثُهَا عِبَادِيَ الصَّالِحُونَ ﴿١٠٥﴾

105. Na kwa yakini Tuliandika katika Vitabu Vilivyoteremshwa baada ya (kuandikwa katika) Al-Lawh Al-Mahfuwdh (Ubao Uliohifadhiwa) ya kwamba ardhi watairithi Waja Wangu wema.

 

 

 

إِنَّ فِي هَـٰذَا لَبَلَاغًا لِّقَوْمٍ عَابِدِينَ ﴿١٠٦﴾

106. Hakika katika hii (Qur-aan) bila shaka kuna ujumbe maridhawa kwa watu wenye kuabudu.

 

 

 

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٧﴾

107. Na Hatujakutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni rehma kwa walimwengu.  

 

 

قُلْ إِنَّمَا يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٠٨﴾

108. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika nimefunuliwa Wahy kwamba: Mwabudiwa wenu wa haki ni Ilaah Mmoja. Basi je, nyinyi mumesilimu?

 

 

 

فَإِن تَوَلَّوْا فَقُلْ آذَنتُكُمْ عَلَىٰ سَوَاءٍ ۖ وَإِنْ أَدْرِي أَقَرِيبٌ أَم بَعِيدٌ مَّا تُوعَدُونَ ﴿١٠٩﴾

109. Na kama wakikengeuka, basi sema: Nimekutangazieni sawasawa, na wala sijui ni yako karibu au baidi yale mnayoahidiwa.

 

 

 

إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ مِنَ الْقَوْلِ وَيَعْلَمُ مَا تَكْتُمُونَ ﴿١١٠﴾

110. Hakika Yeye Anajua kauli za kutamkwa jahara, na Anajua mnayoyaficha.

 

 

 

وَإِنْ أَدْرِي لَعَلَّهُ فِتْنَةٌ لَّكُمْ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ ﴿١١١﴾

111. Na wala sijui kama hii huenda ikawa ni mtihani kwenu na starehe mpaka muda fulani.

 

 

 

قَالَ رَبِّ احْكُم بِالْحَقِّ ۗ وَرَبُّنَا الرَّحْمَـٰنُ الْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ ﴿١١٢﴾

112. Akasema: Rabb wangu! Hukumu kwa haki. Na Rabb wetu ni Ar-Rahmaan Aombwaye msaada juu ya yale mnayovumisha.

 

 

 

 

[1] Makafiri Kumpachika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  Sifa Ovu:

 

Rejea Al-Furqaan (25:4), na Asw-Swaaffaat (37:36).

 

[2] Haiwezekani Kuweko Waabudiwa Na Waumbaji Zaidi Ya Mmoja:

 

Rejea Al-Muuminuwn (23:91).

 

[3] Rusuli Wote Wamekuja Kulingania Tawhiyd:

 

Rejea Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى): An-Nahl (16:36), Az-Zukhruf (43:45).

 

[4] Kumsingizia Allaah (سبحانه وتعالى)  Kuwa Kajifanyia Mwana:

 

Rejea Maryam (19:88), Al-Baqarah (2:116), An-Nisaa (4:171), At-Tawbah (9:30)

 

[5] Ash-Shafaa (Uombezi) Kwa Ambaye Tu Allaah (سبحانه وتعالى) Amemridhia:

 

Rejea An-Najm (53:26), Yuwnus (10:3), Maryam (19:87), Twaahaa (20:109), Saba-a (34:23), Az-Zumar (39:44).

 

[6] Mbingu Na Ardhi Zilikuwa Zimeunganishwa:

 

Je, hawaoni ya kwamba mbingu na ardhi ziliunganishwa! Yaani, hapo mwanzo zilikuwa kipande kimoja, zimeshikamana na zimerundikana juu ya kila kitu, kisha Allaah (سبحانه وتعالى)  Akazitenganisha baina yao, na Akazifanya mbingu kuwa saba, na ardhi saba, Akatenganisha baina yao kwa hewa, kisha Akateremsha mvua kutoka mbinguni na kuotesha mimea kutoka ardhini. Na ndipo Anaendelea kusema:

وَجَعَلْنَا مِنَ الْمَاءِ كُلَّ شَيْءٍ حَيٍّ ۖ  

Na Tukajaalia kutokana na maji kila kitu kilicho hai.”

 

Sufyaan Ath-Thawriy amesimulia kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ‘Ikrimah kwamba Ibn ‘Abbaas aliulizwa: “Je usiku ulikuwa kabla ya mchana?” Akasema: Kwani hamjui kwamba

  السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ كَانَتَا رَتْقًا فَفَتَقْنَاهُمَا ۖ

Mbingu na ardhi zilikuwa zimeshikamana.”

 

Si kulikuwa na kiza tu baina yao? Hivyo ili mjue kwamba usiku ulikuwa kabla ya mchana.” [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

[7] Mzunguko Maalumu Wa Sayari Angani.

 

[8] Makafiri Wamekanusha Jina La Ar-Rahmaan:

 

Rejea Al-Israa (17:110), Al-Furqaan (25:60).

 

[9] Ada Ya Makafiri Kuuliza Lini Adhabu Itawafikia Au Lini Qiyaamah Kitatokea:

 

Rejea Yuwnus (10:48).

 

[10] Kupunguzwa Ncha Ya Ardhi:

 

Yaani, kwa kufa watu wake na kutoweka kwao, kidogo kidogo, mpaka Allaah (سبحانه وتعالى) Airithi ardhi na walio juu yake, Naye Ndiye Mbora wa Warithi. Na lau wangelitambua hali hii, basi wasingelidanganyika na kuendelea  na hali zao walizonazo. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[11] Hakuna Amali Inayosahaulika Kwa Allaah (سبحانه وتعالى) Iwe Njema Au Ovu:

 

Rejea Az-Zalzalah (99:7-8), An-Nisaa (4:40), Yuwnus (10:61), Saba-a (34:22).

 

[12]  Duaa Ya Nabiy Ibraahiym Alipokuwa Anaingizwa Katika Moto:

 

Rejea Aal-‘Imraan (3:173).

 

[13] Moto Uliamrishwa Uwe Baridi Na Salama:

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Lau Allaah (عزّ وجلّ) Asingelisema “Na Salama”, basi moto ungelimdhuru Ibraahiym kutokana na ubaridi wake mkali. Na Salaf wengineo wamenukuu kama hivo. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Qataadah amesema: "Siku hiyo hakikuweko kiumbe kisichojaribu kuuzima moto wa Ibraahiym (عليه السّلام) ila mjusi."  Na Hadiyth imethibitisha:

 

حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، أَوِ ابْنُ سَلاَمٍ عَنْهُ أَخْبَرَنَا ابْنُ جُرَيْجٍ، عَنْ عَبْدِ الْحَمِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيَّبِ، عَنْ أُمِّ شَرِيكٍ ـ رضى الله عنها أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَمَرَ بِقَتْلِ الْوَزَغِ وَقَالَ ‏ "‏ كَانَ يَنْفُخُ عَلَى إِبْرَاهِيمَ عَلَيْهِ السَّلاَمُ ‏"‏‏.‏

Amesimulia Umm Shariyk (رضي الله عنها): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameamuru mjusi auliwe akasema: Alikuwa akipuliza (moto) kwa Ibraahiym (عليه السّلام).” [Al-Bukhaariy]

 

[14] Ardhi Ya Shaam Iliyobarikiwa:

 

Miongoni mwa baraka za Sham, ni wingi wa Manabii waliokuweko humo. Na Allaah (سبحانه وتعالى)  Ameichagua kwa ajili ya Khaliyl Wake Ibraahiym (عليه السّلام)  ahajiri huko. Na humo mna mojawapo ya Nyumba Zake tukufu tatu, nayo ni Bayt Al-Maqdis: [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[15] Janga Kuu:

 

Ni maudhi, mashaka, shida, kukadhibishwa kwa muda wa miaka mia tisa na khamsini akilingania watu wake katika Tawhiyd, na hawakuamini isipokuwa wachache tu.

 

[16] Dhul-Kifl Ni Nabiy Au Mja Mwema:

 

 ‘Ulamaa wamekhitilafiana katika kauli mbili kama ni Nabiy au ni mja mwema, na kauli iliyo na nguvu zaidi ni kwamba, Dhul-Kifl ni Nabiy kutokana na kutajwa kwake pamoja na Manabii (katika Suwrah hii na Suwrah Swaad 38:48). [Tafsiyr Ibn Kathiyr] Na Allaah Ni Mjuzi zaidi.

 

[17] Duaa Yenye Kutaqabaliwa Haja:

 

 عَنْ سَعْدٍ بن أبي وقاص (رضي الله عنه)  قَالَ:  قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم)َ: ((دَعْوَةُ ذِي النُّونِ إِذْ دَعَا وَهُوَ فِي بَطْنِ الْحُوتِ: "لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنْتُ مِنْ الظَّالِمِينَ" فَإِنَّهُ لَمْ يَدْعُ بِهَا رَجُلٌ مُسْلِمٌ فِي شَيْءٍ قَطُّ إِلاَّ اسْتَجَابَ اللَّهُ لَهُ))

Amesimulia Sa’d bin Abiy Waqqaasw (رضي الله عنه):  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Duaa ya Dhan-Nuwn (Nabiy Yuwnus)  alipoomba alipokuwa katika tumbo la nyangumi:

لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنْتُ مِنْ الظَّالِمِينَ

Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Utakasifu ni Wako, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.

Basi hakika hakuna Muislamu aombaye kwayo kitu chochote kile ila Allaah Atamuitikia.” [Swahiyh At-Tirmidhiy (3505), Swahiyh Al-Jaami’ (3383), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (1744)]

 

[18] Sifa Ya Waumini Wanapotenda Mema Huwa Baina Ya Khofu Na Matarajio:

 

Rejea Al-Muuminuwn (23:60-61).

 

[19] Yaajuwj Na Maajuwj Ni Katika Alama Kubwa Za Qiyaamah:

 

Rejea Al-Kahf (18:93-99).

 

Hili ni tahadharisho la Allaah (سبحانه وتعالى) kwa watu kwamba wasije wakang'ang'ania ukafiri na maasi, kwani wakati umekaribia wa kudhihiri Yaajuwj na Maajuwj. Haya ni makabila mawili makubwa ya wana wa Aadam. Dhul-Qarnayn alijenga kizuizi cha kuwazuia, wakati aliposhitakiwa juu ya uharibifu wao katika ardhi. Na katika nyakati za mwisho (Alama kubwa za Qiyaamah kama inavyotaja Aayah inayofuatia (97), kizuizi kitavunjwa na watajitokea kwa nguvu kwa watu kutoka kila pande za mnyanyuko, kwa namna Aliyoelezea Allaah (سبحانه وتعالى). Hii ni dalili juu ya idadi yao kubwa mno, na kasi kubwa watakayozunguka nayo duniani kote, kutokana na ima nguvu zao wenyewe au kutokana na nyenzo ambazo  Allaah (سبحانه وتعالى) Atawaumbia. Ina maana kwamba watakuwa na uwezo wa kuvuka masafa makubwa, na kufanya yaliyo magumu kwao yawe ni mepesi. Na kwamba watawatawala watu na kuwakandamiza katika dunia, na kwamba hapatakuwa na mwenye uwezo wa kupigana nao. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[20] Makafiri Kuifahamu Ndivyo Sivyo

Kauli Ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمْ لَهَا وَارِدُونَ ﴿٩٨﴾

Hakika nyinyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah ni vichochezi vya moto wa Jahannam, nyinyi mtauingia.

 

Makafiri wa ki-Quraysh wa Makkah waliifahamu ndivyo sivyo Aayah hii kwamba, wanaoabudiwa wote, wakiwemo masanamu yao. Na pia wakawahusisha waja wa Allaah (سبحانه وتعالى) kama mja mwema ‘Uzayr, aliyekuwa akiabudiwa na Mayahudi, na Nabiy ‘Isyaa (عليه السّلام) aliyekuwa akiabudiwa na Manaswara, kwamba wamo katika hukmu hii, yaani, wawe vichochezi vya moto wa Jahannam pamoja na wao wanawaabudu.  Washirikina walimwendea Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kumfanyia kejeli kwa hayo lakini Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha Aayah kuwajibu washirikina wa Makkah.

 

Rejea Alhidaaya.com

 

021-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Anbiyaa Aayah 101: إِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمْ لَهَا وَارِدُونَ

 

Basi ufahamu huo ulikuwa wa batili kwa sababu Aayah hiyo ilikuwa inawaelekezea washirikina wa Makkah na masanamu yao waliyokuwa wakiyaabudu. Na ‘Ulamaa wamefafanua Aayah hii kwa maelezo bayana.  Na hii ni radd pia kwa makafiri wengineo wanaotaka kuitafutia upogo Qur-aan Tukufu kwa akili zao finyu, na inadi zao.

 

Rejea pia Az-Zukhruf (43:57).

 

[21] Sababu Ya Kuteremshwa Aayah:

 

Bonyeza kiungo kifuatacho chenye Sababun-Nuzuwl (Sababu Ya Kuteremshwa) Aayah au Suwrah:

 

043-Asbaabun-Nuzuwl: Az-Zukhruf Aayah 57: وَلَمَّا ضُرِبَ ابْنُ مَرْيَمَ مَثَلا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ

 

Rejea pia Az-Zukhruf (43:57).

 

Ambao Imewatangulia Al-Husnaa (Furaha, Rehma) Ya Allaah (عزّ وجلّ):

 

Ni utangulizi wa furaha katika ilimu ya Allaah na katika Al-Lawh Al-Mahfuwdhw (Ubao Uliohifadhiwa) katika usahilishaji wao hapa duniani kwa ajili ya wepesi na matendo mema. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

Hao ni wema wa Allaah; Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام), ‘Uzayr, Malaika, na wengineo ambao wameabudiwa bila ya wao kuridhia. Na Aayah hii inahusiana na Aayah iliyotangulia (98) ambayo washirikina walidai kuwa, hawa nao wataingia Jahannam wawe vichochezi vya moto. Basi hawa hawataadhibiwa. Na  ndio wanaingia katika Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) ya Aayah hii ya (101) na zinazofuatia (102-103).

 

[22] Sahifa (Kurasa) Za Matendo Maovu Aliyoyatenda Kila Mmoja Duniani:

 

Rejea Al-Israa (17:13), Al-Haaqqah (69:19-29), Al-Inshiqaaq (84:7-15), Az-Zalzalah (99).

 

 حَدَّثَنَا سُوَيْدُ بْنُ نَصْرٍ، أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ لَيْثِ بْنِ سَعْدٍ، حَدَّثَنِي عَامِرُ بْنُ يَحْيَى، عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ الْمَعَافِرِيِّ، ثُمَّ الْحُبُلِيِّ قَالَ سَمِعْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ، يَقُولُ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ إِنَّ اللَّهَ سَيُخَلِّصُ رَجُلاً مِنْ أُمَّتِي عَلَى رُءُوسِ الْخَلاَئِقِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَيَنْشُرُ عَلَيْهِ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ سِجِلاًّ  كُلُّ سِجِلٍّ مِثْلُ مَدِّ الْبَصَرِ ثُمَّ يَقُولُ أَتُنْكِرُ مِنْ هَذَا شَيْئًا أَظَلَمَكَ كَتَبَتِي الْحَافِظُونَ فَيَقُولُ لاَ يَا رَبِّ ‏.‏ فَيَقُولُ أَفَلَكَ عُذْرٌ فَيَقُولُ لاَ يَا رَبِّ ‏.‏ فَيَقُولُ بَلَى إِنَّ لَكَ عِنْدَنَا حَسَنَةً فَإِنَّهُ لاَ ظُلْمَ عَلَيْكَ الْيَوْمَ فَتَخْرُجُ بِطَاقَةٌ فِيهَا أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ فَيَقُولُ احْضُرْ وَزْنَكَ فَيَقُولُ يَا رَبِّ مَا هَذِهِ الْبِطَاقَةُ مَعَ هَذِهِ السِّجِلاَّتِ فَقَالَ إِنَّكَ لاَ تُظْلَمُ ‏.‏ قَالَ فَتُوضَعُ السِّجِلاَّتُ فِي كِفَّةٍ وَالْبِطَاقَةُ فِي كِفَّةٍ فَطَاشَتِ السِّجِلاَّتُ وَثَقُلَتِ الْبِطَاقَةُ فَلاَ يَثْقُلُ مَعَ اسْمِ اللَّهِ شَيْءٌ ‏"‏ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ ‏.‏حَدَّثَنَا قُتَيْبَةُ، حَدَّثَنَا ابْنُ لَهِيعَةَ، عَنْ عَامِرِ بْنِ يَحْيَى، بِهَذَا الإِسْنَادِ نَحْوَهُ بِمَعْنَاهُ ‏.‏ وَالْبِطَاقَةُ هِيَ الْقِطْعَةُ ‏.‏

Amesimulia ‘Abdullaah Bin ‘Amr Bin Al-‘Aasw (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Atampambanua mtu katika ummah wangu  mbele ya viumbe vyote siku ya Qiyaamah. Atakunjuliwa Sahifa (kurasa) tisini na tisa (za matendo maovu ya duniani), kila sahifa itakuwa ndefu kadiri ya jicho linavyoweza kuona. Kisha (Allaah) Atasema: Je! Unakanusha jambo lolote katika haya? Je! Waandishi Wangu (Malaika) wamekudhulumu kitu humo? (Mtu huyo) atasema: Hapana ee Rabb! (Allaah) Atasema: Je, una udhuru wowote? Atasema: Hapana ee Rabb! (Allaah) Atasema: Bali unalo jambo jema Kwetu, kwani leo hutodhulumiwa! Kisha Atatoa kadi ndani yake imeandikwa:

 

أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ

Ninashuhudia kwamba laa ilaaha illa-Allaah, na ninashuhudia kwamba Muhammad ni Mja Wake na Rasuli Wake.

 

(Allaah) Atasema: Lete mizani yako. Atasema: Ee Rabb! Je, kadi hii ina thamani gani mbele ya sahifa hizo? (Allaah) Atasema: Hakika hutodhulumiwa. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Sahifa (zilorekodi amali) zitawekwa juu ya sahani mojawapo ya sahani mbili za mizani na kadi itawekwa katika sahani nyengineyo. Basi sahifa zitakuwa nyepesi katika mizani na kadi itakuwa nzito. Hakuna chochote kitakachokuwa kizito zaidi kuliko Jina la Allaah.” [At-Tirmidhiy, Sunan Ibn Maajah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (1533)

 

[23]  Watu Watafufuliwa Katika Umbo La Awali Kama Walivyozaliwa:

 

Rejea Al-Kahf  (18:48), Al-An’aam (6:94). Na Hadiyth ifuatayo inaelezea hali za watu watakavyofufuliwa Siku hiyo ya Qiyaamah na watu wengine watakaokanwa kwa sababu ya kuzusha mambo katika Dini. 

 

‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما)   amesema: Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama na kututolea mawaidha akasema: “Enyi watu, hakika mtafufuliwa na Allaah hali ya kuwa hamna viatu, mpo uchi na bila kutahiriwa  (na magovi). (Akasoma) Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُ

“Kama Tulivyoanza umbo la awali Tutalirudisha tena.” [Al-Anbiyaa: (104)]

 

Tanabahini! Hakika mtu wa kwanza atakayevishwa nguo ni Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام). Tanabahini! Wataletwa watu katika Ummah wangu na watapelekwa upande wa kushoto (motoni), nami nitasema: “Ee Rabb wangu, Swahaba wangu!” Nitaambiwa: “Wewe hujui watu hawa walichokizua baada yako.” Hapo nitasema kama alivyosema mja mwema (Nabiy ‘Iysaa):

 

وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿١١٧﴾

“Na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao. Uliponikamilishia muda Ukanichukua juu, Ulikuwa Wewe Ndiye Mwangalizi juu yao. Na Wewe Ni Mwenye Kushuhudia kila kitu.”

 

إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾

“Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni Waja Wako, na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.” [Al-Maaidah (5:117-118]

 

Nitaambiwa: “Wao waliendelea kukengeuka na kugeuka nyuma kuondokelea mbali ulipowaacha.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Share