065 - Atw-Twalaaq
الطَّلاق
065-Atw-Twalaaq
065-Atw-Twalaaq: Utangulizi Wa Suwrah
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ رَبَّكُمْ ۖ لَا تُخْرِجُوهُنَّ مِن بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخْرُجْنَ إِلَّا أَن يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُّبَيِّنَةٍ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ ۚ لَا تَدْرِي لَعَلَّ اللَّـهَ يُحْدِثُ بَعْدَ ذَٰلِكَ أَمْرًا﴿١﴾
1. Ee Nabiy! Mtakapowataliki wanawake, basi watalikini katika wakati wa eda (twahaarah) zao, na hesabuni barabara eda, na mcheni Allaah Rabb wenu. Msiwatowe katika nyumba zao, na wala wao wasitoke isipokuwa wakileta uchafu ulio bayana. Na hiyo ndio Mipaka ya Allaah. Na yeyote atakayevuka Mipaka ya Allaah, basi kwa yakini amedhulumu nafsi yake. Hujui; huenda Allaah Atatokezesha jambo jingine baada ya haya.[1]
فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِّنكُمْ وَأَقِيمُوا الشَّهَادَةَ لِلَّـهِ ۚ ذَٰلِكُمْ يُوعَظُ بِهِ مَن كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا﴿٢﴾
2. Na watakapokaribia kufikia muda wao (wa eda), basi wazuieni kwa wema, au farikianeni nao kwa wema, na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu, na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Allaah. Hivyo ndivyo anavyowaidhiwa anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na yeyote anayemcha Allaah[2], basi Atamfanyia njia ya kutoka (shidani).
وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ ۚ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ فَهُوَ حَسْبُهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بَالِغُ أَمْرِهِ ۚ قَدْ جَعَلَ اللَّـهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا﴿٣﴾
3. Na Atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii. Na yeyote anayetawakali kwa Allaah, basi Yeye Humtosheleza. Hakika Allaah Anatimiza Kusudio Lake. Allaah Amejaalia makadirio kwa kila kitu.[3]
وَاللَّائِي يَئِسْنَ مِنَ الْمَحِيضِ مِن نِّسَائِكُمْ إِنِ ارْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَاثَةُ أَشْهُرٍ وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ ۚ وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مِنْ أَمْرِهِ يُسْرًا﴿٤﴾
4. Na wale wanawake wanaokoma hedhi miongoni mwa wanawake wenu, mkiwa mna shaka, basi eda yao ni miezi mitatu, pamoja na wale wanawake wasiopata hedhi. Na wenye mimba muda wao (wa eda) watakapozaa mimba zao.[4] Na yeyote anayemcha Allaah basi Atamjaalia wepesi katika jambo lake.
ذَٰلِكَ أَمْرُ اللَّـهِ أَنزَلَهُ إِلَيْكُمْ ۚ وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّئَاتِهِ وَيُعْظِمْ لَهُ أَجْرًا﴿٥﴾
5. Hiyo ni Amri ya Allaah Amekuteremshieni. Na yeyote anayemcha Allaah, basi Atamfutia maovu yake na Atamuadhimishia ujira.
أَسْكِنُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ سَكَنتُم مِّن وُجْدِكُمْ وَلَا تُضَارُّوهُنَّ لِتُضَيِّقُوا عَلَيْهِنَّ ۚ وَإِن كُنَّ أُولَاتِ حَمْلٍ فَأَنفِقُوا عَلَيْهِنَّ حَتَّىٰ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ فَإِنْ أَرْضَعْنَ لَكُمْ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۖ وَأْتَمِرُوا بَيْنَكُم بِمَعْرُوفٍ ۖ وَإِن تَعَاسَرْتُمْ فَسَتُرْضِعُ لَهُ أُخْرَىٰ﴿٦﴾
6. Wawekeni wanawake (mliowataliki) kwenye majumba mnayokaa nyinyi kwa kadiri ya kipato chenu, na wala msiwadhuru ili muwatie dhiki. Na wakiwa ni wenye mimba, basi wapeni matumizi mpaka wazae mimba zao. Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao. Na shaurianeni baina yenu kwa wema. Na mkifanyiana uzito, basi amnyonyeshee mwanamke mwengine.
لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِ ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّـهُ ۚ لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا مَا آتَاهَا ۚ سَيَجْعَلُ اللَّـهُ بَعْدَ عُسْرٍ يُسْرًا﴿٧﴾
7. Ili mwenye wasaa agharimu kwa wasaa wake, na aliyebaniwa riziki yake, basi agharimie katika kile Alichompa Allaah.[5] Allaah Haikalifishi nafsi yeyote ile isipokuwa kwa kile Alichoipa. Allaah Atajaalia baada ya ugumu kuwa wepesi.
وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ عَتَتْ عَنْ أَمْرِ رَبِّهَا وَرُسُلِهِ فَحَاسَبْنَاهَا حِسَابًا شَدِيدًا وَعَذَّبْنَاهَا عَذَابًا نُّكْرًا﴿٨﴾
8. Na miji mingapi imeasi Amri ya Rabb wake na Rusuli Wake, basi Tuliihisabia hisabu shadidi, na Tukaiadhibu adhabu kali kabisa isiyovumilika.
فَذَاقَتْ وَبَالَ أَمْرِهَا وَكَانَ عَاقِبَةُ أَمْرِهَا خُسْرًا﴿٩﴾
9. Ikaonja maovu ya mambo yake, na ikawa hatima ya mambo yake kuwa ni khasara.
أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ يَا أُولِي الْأَلْبَابِ الَّذِينَ آمَنُوا ۚ قَدْ أَنزَلَ اللَّـهُ إِلَيْكُمْ ذِكْرًا﴿١٠﴾
10. Allaah Amewaandalia adhabu shadidi, basi mcheni Allaah enyi wenye akili mlioamini! Allaah Amekwishakuteremshieni Ukumbusho.
رَّسُولًا يَتْلُو عَلَيْكُمْ آيَاتِ اللَّـهِ مُبَيِّنَاتٍ لِّيُخْرِجَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ ۚ وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُدْخِلْهُ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ قَدْ أَحْسَنَ اللَّـهُ لَهُ رِزْقًا﴿١١﴾
11. Ni Rasuli anakusomeeni Aayaat za Allaah zinazobainisha, ili kuwatoa wale walioamini na wakatenda mema kutoka kwenye viza kuingia katika Nuru.[6] Na yeyote anayemwamini Allaah na akatenda mema, Atamuingiza Jannaat zipitazo chini yake mito wadumu humo abadi. Allaah Amekwishamfanyia rizki nzuri kabisa.
اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ وَمِنَ الْأَرْضِ مِثْلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ الْأَمْرُ بَيْنَهُنَّ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَأَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ عِلْمًا﴿١٢﴾
12. Allaah ni Yule Aliyeumba mbingu saba na katika ardhi mfano wa hizo[7], inateremka amri baina yao ili mjue kwamba Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza, na kwamba Allaah Amekwishakizunguka kila kitu kwa Ujuzi (Wake).
[1] Talaka:
Aayah hii namba (1) Atw-Twalaaq hadi Aayah namba (7) zinahusiana na mas-ala ya talaka, eda ya talaka na ya mfiwa, ambayo hukmu zake zimetajwa pia katika Suwrah Al-Baqarah kuanzia Aayah namba (226) hadi Aayah namba (237). Na pia (2:241). Rejea pia Al-Ahzaab (33:49).
Tafsiyr ya Aayah:
Ee Nabiy! Pindi mnapotaka, wewe na Waumini, kuwapa talaka wake zenu, basi wapeni talaka wakiwa kwenye hali ya kukabili kipindi cha wao kukaa eda- yaani kwenye hali ya usafi ambao hakukupatikana kuingiliwa, au katika hali ya mimba iliyo wazi- na mshike hesabu ya eda, mpate kujua muda wa kuwarejea iwapo mtataka kuwarejea, na muogopeni Allaah (سبحانه وتعالى) Rabb wenu. Wala msiwatoe wanawake waliopewa talaka kwenye majumba wanayokaa mpaka eda lao limalizike, nalo ni hedhi tatu kwa asiyekuwa mdogo (asiyeingia damuni) na si kwa aliyekata tamaa ya kuingia damuni (kwa uzee) wala mwenye mimba. Na haifai kwa wanawake hao kutoka majumbani mwao wao wenyewe isipokuwa watakapofanya kitendo kiovu cha waziwazi kama vile uzinifu. Na hizo ndizo hukumu za Allaah Alizozipitisha kwa Waja Wake. Na Mwenye kuzikiuka hukumu za Allaah, basi huyo amejidhulimu nafsi yake na ameipeleka mahali pa maangamivu. Hujui, ee mtoaji talaka, kwamba Allaah huenda, baada ya talaka hiyo, Akaleta jambo usilolitazamia ukaja ukamrudia. [Tafsiyr Al-Muyassar]
Na Hadiyth ifuatayo imethibitisha kuhusu mwanamke kutalikiwa akiwa katika twahara:
حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، قَالَ حَدَّثَنِي عُقَيْلٌ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي سَالِمٌ، أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عُمَرَ ـ رضى الله عنهما ـ أَخْبَرَهُ أَنَّهُ، طَلَّقَ امْرَأَتَهُ وَهْىَ حَائِضٌ، فَذَكَرَ عُمَرُ لِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَتَغَيَّظَ فِيهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ قَالَ " لِيُرَاجِعْهَا ثُمَّ يُمْسِكْهَا حَتَّى تَطْهُرَ، ثُمَّ تَحِيضَ فَتَطْهُرَ، فَإِنْ بَدَا لَهُ أَنْ يُطَلِّقَهَا فَلْيُطَلِّقْهَا طَاهِرًا قَبْلَ أَنْ يَمَسَّهَا فَتِلْكَ الْعِدَّةُ كَمَا أَمَرَهُ اللَّهُ ".
Amesimulia Saalim (رضي الله عنه): ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنهما) amemwambia kuwa alimtaliki mkewe akiwa katika hedhi, kwa hiyo, ‘Umar (رضي الله عنه) akamtajia hilo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikasirika sana kwa jambo hilo, kisha akasema: “Ni lazima (Ibn ‘Umar) amrejee, kisha amuweke kama mkewe mpaka atwahirike, kisha aingie tena katika hedhi kisha atwahirike. Baada ya hapo, ikiwa anataka kumtaliki anaweza kufanya hivyo akiwa mkewe yuko katika hali ya twahara kabla ya kumgusa. Hiyo ndio eda kama Alivyoamrisha Allaah.”
Bonyeza viungo viungo vifuatavyo kupata faida:
07-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Talaka
08-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa (Talaka Ya) Rejea
68-Al-Bukhaariy Kitabu Cha Talaka - كتاب الطلاق
Eda: Hikma Yake, Hukmu Zake, Yanayopasa Na Yasiyopasa
11-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa: Al-‘Iddah (Kukaa Eda) Na Al-Ihdaad (Matanga)
06-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Mlango Wa Khul’
[2] Taqwa:
Rejea Al-Baqarah (2:2) kwenye maana ya taqwa. Rejea pia viungo vifuatavyo kuhusu maamrisho ya taqwa, faida na fadhila zake:
006-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Taqwa – Kumkhofu Allaah
021-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kusaidiana Katika Wema Na Taqwa
Maana Ya Taqwa
Faida Ya Taqwa (Uchaji Allaah)
[3] Anayetawakkal Kwa Allaah, Allaah Atamtosheleza Kwa Kila Kitu:
عن ابنِ عباسٍ رضي الله عنهما، قَالَ: كنت خلف النَّبيّ صلى الله عليه وسلم يومًا، فَقَالَ: ((يَا غُلامُ، إنِّي أعلّمُكَ كَلِمَاتٍ: احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجَاهَكَ، إِذَا سَألْتَ فَاسأَلِ الله، وإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ باللهِ. وَاعْلَمْ: أنَّ الأُمَّةَ لَوْ اجْتَمَعَتْ عَلَى أنْ يَنْفَعُوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبهُ اللهُ لَكَ، وَإِن اجتَمَعُوا عَلَى أنْ يَضُرُّوكَ بِشَيءٍ لَمْ يَضُرُّوكَ إلا بِشَيءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الأَقْلاَمُ وَجَفَّتِ الصُّحفُ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث حسن صحيح)).
وفي رواية غيرِ الترمذي: ((احْفَظِ الله تَجِدْهُ أَمَامَكَ، تَعرَّفْ إِلَى اللهِ في الرَّخَاءِ يَعْرِفكَ في الشِّدَّةِ، وَاعْلَمْ: أنَّ مَا أَخْطَأكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبكَ، وَمَا أصَابَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ، وَاعْلَمْ: أنَّ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ، وَأَنَّ الفَرَجَ مَعَ الكَرْبِ، وَأَنَّ مَعَ العُسْرِ يُسْرًا))
Amesimulia ‘Abdullaah Bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Siku moja nilikuwa (juu ya mnyama) nyuma ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniambia: “Ee kijana, mimi nitakufundisha maneno: Mhifadhi Allaah Naye Atakuhifadhi. Mhifadhi Allaah utamkuta yupo mbele yako. Unapoomba, muombe Allaah. Unapotaka msaada, mtake Allaah. Fahamu kuwa, lau ummah (wote) utajikusanya ili wakunufaishe kwa jambo, basi hawataweza kukunufaisha ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah; na wakijumuika ili wakudhuru kwa jambo, hawataweza kukudhuru ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah. Kalamu zimeshasimama na karatasi zimeshakauka.” [At-Tirmidhiy, na amesema: Hadiyth Hasan Swahiyh]
Riwaayah nyingine isiyokuwa ya At-Tirmidhiy imesema:
“Mhifadhi Allaah utamkuta Yupo mbele yako. Mjue Allaah katika raha Naye Atakujua katika shida. Ujue kuwa, lililokukosa halikuwa ni lenye kukupata, na lililokusibu halikuwa ni lenye kukukosa. Ujue kuwa nusura ipo pamoja na subira, faraja ipo pamoja na dhiki, na kwenye uzito kuna wepesi.”
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida nyenginezo:
007-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Yakini Na Kutawakali Kwa Allaah
006-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Kutawakali Kwa Allaah Na Kuwa Na Moyo Laini
067-Du'aa Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kujisalimisha Kwa Allaah, Kumwamini, Kutawakali Kwake, Kutubia Kwake...
[4] Eda Ya Mwanamke Mwenye Mimba Na Aliyefiwa Na Mumewe:
Eda ni muda wa kusubiri ambapo mwanamke haruhusiwi kuolewa, baada ya kifo cha mumewe au kuachika.
Kwa mwanamke mwenye mimba, katika hali yoyote iwe ni kifo cha mumewe au kuachika, eda yake ni baada ya kuzaliwa mtoto. Kwa mfano ameachika au mumewe amefariki leo, na siku inayofuata akajifungua mtoto, eda yake huisha kwa kuzaliwa mtoto. Hapo anaruhusiwa kuolewa wakati wowote, lakini kwa muda wote ambapo atakuwa yupo katika nifaas hatoruhusiwa kuingiliwa na mumewe.
Na Hadiyth ifuatayo imethibitisha:
حَدَّثَنَا سَعْدُ بْنُ حَفْصٍ، حَدَّثَنَا شَيْبَانُ، عَنْ يَحْيَى، قَالَ أَخْبَرَنِي أَبُو سَلَمَةَ، قَالَ جَاءَ رَجُلٌ إِلَى ابْنِ عَبَّاسٍ وَأَبُو هُرَيْرَةَ جَالِسٌ عِنْدَهُ فَقَالَ أَفْتِنِي فِي امْرَأَةٍ وَلَدَتْ بَعْدَ زَوْجِهَا بِأَرْبَعِينَ لَيْلَةً. فَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ آخِرُ الأَجَلَيْنِ. قُلْتُ أَنَا وَأُولاَتُ الأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَنْ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ أَنَا مَعَ ابْنِ أَخِي ـ يَعْنِي أَبَا سَلَمَةَ ـ فَأَرْسَلَ ابْنُ عَبَّاسٍ غُلاَمَهُ كُرَيْبًا إِلَى أُمِّ سَلَمَةَ يَسْأَلُهَا فَقَالَتْ قُتِلَ زَوْجُ سُبَيْعَةَ الأَسْلَمِيَّةِ وَهْىَ حُبْلَى، فَوَضَعَتْ بَعْدَ مَوْتِهِ بِأَرْبَعِينَ لَيْلَةً فَخُطِبَتْ فَأَنْكَحَهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَكَانَ أَبُو السَّنَابِلِ فِيمَنْ خَطَبَهَا.
Amesimulia Yahya (رضي الله عنه): Abu Salamah alinipasha khabari kwamba, alikuja mtu kwa Ibn ‘Abbaas na Abu Hurayrah (رضي الله عنهما) walikuwa wamekaa mbele yake; mtu yule akasema: Nipe fatwa kuhusu mwanamke aliyejifungua baada ya kufariki mumewe kwa siku arubaini. Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) akasema: Eda yake mwisho ni mihula miwili. Mimi (Abu Salamah) nikasema:
وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ
“Na wenye mimba muda wao (wa eda) watakapozaa mimba zao.”
[Atw-Twalaaq (65:4)]. Na Abu Hurayrah (رضي الله عنه) akasema: Mimi niko pamoja na mtoto wa ndugu yangu (anakusudia Abu Salamah). Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) akamtuma kijana wake kwa Ummu Salamah na kumuuliza. Akajibu: Ameuawa mume wa Subay‘ah
Al-Aslamiyyah, akiwa mja mzito, akajifungua baada ya kifo chake kwa siku arubaini, akaposwa. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamuozesha, na Abu Sanaabil alikuwa miongoni mwa waliomposa.” [Al-Bukhaariy Kitabu Cha Tafsiyr (65)]
Na bonyeza viungo vifuatavyo:
11-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa: Al-‘Iddah (Kukaa Eda) Na Al-Ihdaad (Matanga)
234-Aayah Na Mafunzo: Hikma Ya Eda Ya Mjane Kuwa Miezi Minne Na Siku Kumi
[5] Matumizi Katika Kipindi Cha Eda:
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida:
13-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Matumizi
11-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa: Al-‘Iddah (Kukaa Eda) Na Al-Ihdaad (Matanga)
[6] Kutolewa Kwenye Viza Na Kuingiza Katika Nuru:
Rejea Suwrah Ibraahiym (!4:1) kwenye uchambuzi na rejea mbalimbali za kuhusu maudhui hii.
[7] Mbingu Saba Na Ardhi Saba:
Allaah (سبحانه وتعالى) Amethibitisha kuumba mbingu saba katika Kauli Zake kadhaa kwenye Qur-aan. Miongoni mwazo ni Kauli Yake:
الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا ۖ مَّا تَرَىٰ فِي خَلْقِ الرَّحْمَـٰنِ مِن تَفَاوُتٍ ۖ فَارْجِعِ الْبَصَرَ هَلْ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ﴿٣﴾
“Ambaye Ameumba mbingu saba matabaka. Hutaona katika Uumbaji wa Ar-Rahmaan tofauti yoyote. Basi rejesha jicho. Je, unaona mpasuko wowote ule?” [Al-Mulk (67:3)]
Rejea pia Al-Baqarah (2:29), Al-Israa (17:44), Al-Muuminuwn (23:86) Fusw-Swilat (41:12), Nuwh (71:15).
Na pia imethibitishwa katika Hadiyth zilizoelezea safari ya muujiza ya Al-Israa Wal-Mi’raaj. Rejea Al-Israa (17:1).
Na kuhusu ardhi saba imethibitiwha katika Hadiyth ifuatayo:
حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، أَخْبَرَنَا ابْنُ عُلَيَّةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ أَبِي كَثِيرٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِبْرَاهِيمَ بْنِ الْحَارِثِ، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، كَانَتْ بَيْنَهُ وَبَيْنَ أُنَاسٍ خُصُومَةٌ فِي أَرْضٍ، فَدَخَلَ عَلَى عَائِشَةَ فَذَكَرَ لَهَا ذَلِكَ، فَقَالَتْ يَا أَبَا سَلَمَةَ اجْتَنِبِ الأَرْضَ، فَإِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ " مَنْ ظَلَمَ قِيدَ شِبْرٍ طُوِّقَهُ مِنْ سَبْعِ أَرَضِينَ ".
Amesimulia Muhammad Bin Ibraahym Al-Haarith (رضي الله عنه): Kutoka kwa Abu Salamah bin ‘Abdir-Rahman ambaye alikuwa na utesi baina yake na baadhi ya watu kuhusu kipande cha ardhi, hivyo akaenda kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) na kumwambia kuhusu hilo. ‘Aaishah (رضي الله عنها) akamwambia: Ee Abu Salamah! Jiepushe na ardhi hiyo, kwani Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mwenye kudhulumu shubiri moja ya ardhi, hakika Allaah Atamzingirisha na ardhi saba shingoni mwake Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaari na Muslim]