089 - Al-Fajr

 

الْفَجْر

 

089-Al-Fajr

 

 

089-Al-Fajr: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

وَالْفَجْرِ ﴿١﴾

1. Naapa kwa Alfajiri.

 

 

وَلَيَالٍ عَشْرٍ ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa masiku kumi.

 

 

وَالشَّفْعِ وَالْوَتْرِ ﴿٣﴾

3. Na Naapa kwa shufwa na witri.

 

 

وَاللَّيْلِ إِذَا يَسْرِ ﴿٤﴾

4. Na Naapa kwa usiku unapopita.

 

 

هَلْ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِي حِجْرٍ ﴿٥﴾

5. Je, katika hayo pana haja ya kiapo kwa mwenye akili?

 

 

أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ ﴿٦﴾

6. Je, hukuona vipi Rabb wako Alivyowafanya kina ‘Aad?

 

 

إِرَمَ ذَاتِ الْعِمَادِ ﴿٧﴾

7. Wa Iram[1], walio warefu na wenye nguvu (kama nguzo ndefu)?

 

 

الَّتِي لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِي الْبِلَادِ ﴿٨﴾

8. Ambao hawakuumbwa mfano wao katika ardhi.

 

 

وَثَمُودَ الَّذِينَ جَابُوا الصَّخْرَ بِالْوَادِ ﴿٩﴾

9. Na kina Thamuwd ambao walichonga miamba mabondeni?

 

 

وَفِرْعَوْنَ ذِي الْأَوْتَادِ ﴿١٠﴾

10. Na Firawni mwenye askari washupavu na nguvu kubwa.[2]

 

 

 

الَّذِينَ طَغَوْا فِي الْبِلَادِ ﴿١١﴾

11. Ambao wote hao wamevuka mipaka kuasi katika nchi.

 

 

فَأَكْثَرُوا فِيهَا الْفَسَادَ ﴿١٢﴾

12. Wakakithirisha humo ufisadi.

 

 

فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ ﴿١٣﴾

13. Rabb wako Akawamiminia mjeledi wa adhabu.

 

 

إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ ﴿١٤﴾

14. Hakika Rabb wako bila shaka Yu tayari Anaziona nyenendo zao zote. 

 

 

فَأَمَّا الْإِنسَانُ إِذَا مَا ابْتَلَاهُ رَبُّهُ فَأَكْرَمَهُ وَنَعَّمَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَكْرَمَنِ ﴿١٥﴾

15. Basi binaadamu pale Rabb wake Anapomtia mtihanini, Akamkirimu na Akamneemesha, husema: Rabb wangu Amenikirimu.  

 

 

 

وَأَمَّا إِذَا مَا ابْتَلَاهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَهَانَنِ ﴿١٦﴾

16. Ama Anapomtia mtihanini, Akamdhikishia riziki yake, husema: Rabb wangu Amenidunisha.

 

 

كَلَّاۖ بَل لَّا تُكْرِمُونَ الْيَتِيمَ ﴿١٧﴾

17.  Laa hasha! Bali hamuwakirimu mayatima.

 

 

وَلَا تَحَاضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ ﴿١٨﴾

18. Na wala hamhamasishani katika kulisha maskini.

 

 

وَتَأْكُلُونَ التُّرَاثَ أَكْلًا لَّمًّا ﴿١٩﴾

19. Na mnakula urithi ulaji wa kiroho bila kusaza kitu.

 

 

وَتُحِبُّونَ الْمَالَ حُبًّا جَمًّا ﴿٢٠﴾

20. Na mnapenda mali penzi kubwa la kupita kiasi.

 

 

 

كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا ﴿٢١﴾

21. Laa hasha! Pale ardhi itakapo vunjwavunjwa na kupondwapondwa.  

 

 

وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا ﴿٢٢﴾

22. Na Atakapokuja Rabb wako pamoja na Malaika walio safusafu.[3]

 

 

وَجِيءَ يَوْمَئِذٍ بِجَهَنَّمَۚ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ وَأَنَّىٰ لَهُ الذِّكْرَىٰ ﴿٢٣﴾

23. Na italetwa siku hiyo Jahannam. Siku hiyo binaadamu atakumbuka. Lakini kutamfaa nini kukumbuka huko?!   

 

 

يَقُولُ يَا لَيْتَنِي قَدَّمْتُ لِحَيَاتِي ﴿٢٤﴾

24. Atasema: Ee, laiti ningelikadimisha (mazuri) kwa ajili ya uhai wangu (wa Aakhirah).

 

 

فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ ﴿٢٥﴾

25. Basi siku hiyo hakuna yeyote atakayeadhibu kama Kuadhibu Kwake. 

 

 

وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُ أَحَدٌ ﴿٢٦﴾

26. Na wala hakuna yeyote atakayefungisha (madhubuti) kama kufungisha Kwake (waovu).

 

 

يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ ﴿٢٧﴾

27. (Mwema ataambiwa): Ee nafsi iliyotua!

 

 

ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً ﴿٢٨﴾

28. Rejea kwa Rabb wako ukiwa umeridhika na mwenye kuridhiwa (na Allaah).

 

 

فَادْخُلِي فِي عِبَادِي ﴿٢٩﴾

29. Basi ingia katika kundi la Waja Wangu.

 

 

وَادْخُلِي جَنَّتِي ﴿٣٠﴾

30. Na ingia Jannah Yangu.

 

 

Share