Imaam Al-Albaaniy: Hatujakalifishwa Kuzitia Nyoyo Uongofu

 

Hatujakalifishwa Kuzitia Nyoyo Uongofu

 

Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)

 

ِlhidaaya.com

 

 

Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Sisi hatujakalifishwa kuziongoza nyoyo za watu kwenye Haki ambayo tunayowalingania nayo watu.

Bali sisi tumekalifishwa tufanye Da’wah tu.

 

Anasema Allaah Aliyetukuka:

فَلَعَلَّكَ بَاخِعٌ نَّفْسَكَ عَلَىٰ آثَارِهِمْ إِن لَّمْ يُؤْمِنُوا بِهَـٰذَا الْحَدِيثِ أَسَفًا ﴿٦﴾

Basi huenda ukaiangamiza nafsi yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa ajili yao kusikitika kutokuamini kwao usimulizi huu (Qur-aan).  [Al-Kahf:6]

 

 

[Silsilatu Al-Hudaa Wan-Nuwr 730]

 

Share