Kujengea Kaburi Inajuzu?

 

 

Kujengea Kaburi Inajuzu?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Ahsante Kwa Nasaha Za Wiki Lakini Nina Swali 

 

Je Kaburi Lina Faa Kujengewa Kama Ipo Dalili Yeyote Naomba Mnijuze Ahsante

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Haifai kujengea kaburi kwa dalili ya Hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

نْ جَابِرٍ (رضي الله عنه) قَالَ: نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يُجَصَّصَ الْقَبْرُ وَأَنْ يُقْعَدَ عَلَيْهِ وَأَنْ يُبْنَى عَلَيْهِ. مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu)   amesema:  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kaburi kutiwa chokaa (liwe imara), kuketiwa juu yake na kujengewa. [Muslim]

 

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate faida zaidi:

 

129 - Hadiyth Ya 129: Haifai Kutia Chokaa Makaburi Au Kujengea Au Kukalia

Kujengea Makaburi

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share