Mashairi: Aibariki Manani, Tovuti Ya Alhidaaya - 2

Aibariki Manani Tovuti  Ya Alhidaaya - 2

 

 

Abuu Maysarah Saalim bin Ramadhwaan

 

 

 

بسم الله الرحمن الرحيم

 

 

 

Alhidaaya elimu, Manhaji na tabia,

Durus zilo muhimu, za Aqiyda na Sharia,

Vitabu, Swala Swaumu, usikose kuingia,

Aibariki Manani, tovuti ya Alhidaaya.

 

 

 

 

Kauli za Masalafi, zipo tele humo ndani,

Maneno Imam Shafi,  Muhadithi Albani,

Wamepinga ukhurafi, kwa dalili na kanuni,

Aibariki Manani, tovuti ya Alhidaaya.

 

 

 

 

Kauli Wanachuoni, wa kisasa na wakale,

Kwa elimu ya kidini, faida zake ni tele,

Mkumbushe na jirani, mnasihi polepole

Aibariki Manani, tovuti ya Alhidaaya.

 

 

 

 

Nisisahau mapishi, mabarobaro muoe,

Utasoma maandishi, na chakula ukitoe,

Hakuna tena ubishi, faida tukazizoe,

Aibariki Manani, tovuti ya Alhidaaya.

 

 

 

 

Maudhui Qur-ani, ipo na ya Kiswahili,

Sasa wachelea nini, kazisome mara mbili,

Ubainifu yakini, na 'Asbabi Nuzuli'

Aibariki Manani, tovuti ya Alhidaaya. 

 

 

 

Dua ziko mbalimbali, alizoomba Rasuli,

Hawajaacha mahali, wameweka na dalili,

Waacheni majuhali, wachukie wafe mbali,

Aibariki Manani, tovuti ya Alhidaaya.

 

 

 

 

 

Makundi yalopotea, humo yamebainishwa,

Hakuna kujitetea, wameshatahadharishwa,

Ukienda tembelea, uwaone walotishwa,

Aibariki Manani, tovuti ya Alhidaaya.

 

 

 

 

 

Wewe unangoja nini, elimu ya kiganjani,

Haihitaji thamani, wala ugumu huoni,

Wanaongoza wasomi, sasa watu milioni,

Aibariki Manani, tovuti ya Alhidaaya.

 

 

 

 

Kwa maswali na majibu, kaulize ujibiwe,

Na maradhi utatibu, bila ya sharifu ndiwe,

Mashekhe wasiotabu, waulize ujibiwe,

Aibariki Manani, tovuti ya Alhidaaya.

 

 

 

 

 

Kiswahili cha fasaha, tena hakina ugumu,

Huko kapate nasaha, elimu ni kwa nidhamu,

Usijefanya mzaha, kaufute uawamu,

Aibariki Manani, tovuti ya Alhidaaya..

 

 

 

 

Ukazisome Hadithi, zake Mtume Nabia,

Usilipe na theluthi, humo wote Salafia,

Na hakuna muhdathi, ingia takasa nia

Aibariki Manani, tovuti ya Alhidaaya.

 

 

 

 

 

Mada zimepangiliwa, kwa uzuri wa kisasa,

Elimu umelimiwa, kavune muda ni sasa,

Qur ani wasomewa, kwa sauti za kunasa,

Aibariki Manani, tovuti ya Alhidaaya.

 

 

 

 

Nisiache shukurani, kumshukuru Manani,

Aliyewapa imani, kufidisha Waumini,

Utasoma kitandani, simu yako mkononi,

Aibariki Manani, tovuti ya Alhidaaya.

 

 

 

*Na Allaah Ndio Mjuzi.*

 

 

 

Share