Kumpaka Mtoto Mchanga Wanja Au Masizi Usoni Kwa Ajili Kumkinga Na Husda Inafaa

 

Kumpaka Mtoto Mchanga Wanja Au Masizi

Usoni Kwa Ajili Kumkinga Na Husda Inafaa

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Assalam Aleykoum Warrahmatullah Wabarakatu.

Suala langu la kumpaka mtoto mchanga wanja au masizi usoni ili iwe ni kinga kwa macho ya watu na husda ua kumvisha uzi mweusi ni kinga? na kama si kinga tumfanyie nini iwe kinga tumsomee ayatul kursi asubuhi na jioni au? Na kama nimefanya hivyo jee ni shirki? Naomba ufafanuzi haraka sana asanteni Mola akuzidishieni elmu na taqwa AMIN.

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Hakika ni kuwa wanja ni dawa ya macho pekee wala si kinga ya hasadi. Kufanya hivyo, yaani kumpaka mtoto wanja au masizi usoni haifai kishari’ah kwani huko kunaingia katika shirki kwa kuufanya wanja na hayo masizi yanaweza yakamkinga mtoto.

 

Kinga ya mtoto ni kama alivyotufundisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa tunaweza:

 

1.  Mume anapokutana na mkewe wawe watasoma du’aa: "Allaahumma jannibniy-sh Shaytwaana wa jannibish Shaytwaana maa razaqtana. Akiruzukiwa mtoto hatadhurika na Shaytwaan" [al-Bukhaariy].

 

2.     Kuwasomea watoto Suwrah Al-Ikhlaasw na kinga mbili (Al-Falaq na An-Naas). Baada ya hapo kupuliza mkononi mwako na kuwapangusa mwili mzima.

 

3.     Na njia nyingine ni kuwasomea du’aa za kinga kama aliyofanya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa wajukuu zake: "U‘idhukumaa bikalimaatiLlaahi at-Taammaati min kulli Shaytwaaniw wa haammah wa min kulli ‘aynil laammah" [al-Bukhaariy].

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Kuwaosha Watoto Wachanga Kwa Majimbo Kwa Ajili Ya Siha Na Kuwakinga Maovu Inafaa?

 

Vipi Kuwakinga Watoto Na Mashaytwaan?

 

Kuzingua Kwa Kuwekea Nazi Na Kuku Ni Shirk?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share