Hilaal: Afuate Mwandamo Wa Mwezi Nchi Anayoishi Au Unapoandama Nchi Yoyote?

 

Hilaal:  Afuate Mwandamo Wa Mwezi Nchi Anayoishi Au Unapoandama Nchi Yoyote?

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Assalaamu alaikum,

Je nifunge lini,pale mwezi unapoandama sehemu yoyote ya dunia   au mpaka utangazwe na viongozi wa kidini katika Nchi yangu. Kwa leo ni hayo tuu.
Ndugu yenu katika uislam 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kauli iliyo sahihi na yenye nguvu ni kufunga kwa kuonekana popote mwezi. Hadiyth mbalimbali zimeonyesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alifunga kwa taarifa za mwezi kutoka sehemu mbalimbali na vile alifungua kutokana na taarifa zilizomjia bila hata yeye kuuona mwezi. Suala hili ni refu na dalili ni nyingi.

 

Uislam hauna mipaka, na popote duniani Muislam atakapouona mwezi, basi anapaswa Muislam aliyesikia taarifa hizo kufunga bila kujali yuko nchi gani au mji gani. Yasemwayo kuhusu kufunga kwa kiwango cha masafa au kipimo cha vitongoji au ukaribu wa majimbo, miji na nchi, hili halina dalili katika sheria bali ni jitihada za wanachuoni.

 

Na mojawapo ya fadhila za kutekeleza matendo ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  ya kufunga kwa kuonekana mwezi popote, ni kupatikana kwa umoja na mshikamano baina ya Waislam kila sehemu duniani. Na ndipo panapoweza vilevile kupatikana siku moja ya 'Iyd duniani na Waislam wote wakawa katika furaha na sherehe pamoja.

 

Hata hivyo, kuna baadhi ya Wanachuoni wanaoonelea kila mtu afunge na mwezi wa nchi yake au utakaotangazwa na Kiongozi wa Kiislamu wa nchi yake.

 

Kifupi, haya mas-alah yana ikhtilaaf na haipaswi upande mmoja kuwalaumu wengine au kuwabeza.

 

Kwa faida ziyada bonyeza viungo vifuatavyo:

 

Hilaal: Kila Mji Ufuate Mwezi Unapoonekena Kwao Au Mwandamo Wa Kimataifa?

 

Hilaal: Kufuata Mwezi Wa Kitaifa Au Wa Kimataifa, Zamani Walipataje Khabari Za Mwandamo?

 

Hilaal: Kumfuata Mume Kwa Msimamo Wa Mwezi Wa Kitaifa

 

Hilaal: Kuonekana Kwa Mwezi Sehemu Tofauti Na Kuanza Swawm

 

Hilaal: Mwandamo Wa Mwezi Upi Sahihi Wa Kitaifa Au Kimataifa?

 

Hilaal: Mwezi Ulionekana Siku Moja Nchi Nyingine Mapema Zaidi Yetu Je, Tulipe Siku Hiyo?

 

Hilaal: Nilifunga Na Waliochelewa Kuanza Swawm Nikasafiri Nikafika Siku Ya ‘Iyd Niendelee Swawm?

 

Hilaal: Tunaambiwa Wanaofuata Mwezi Wa Kimataifa Wamekosea Na Walipe Swawm, Ni Sawa?

 

Hilaal: Utata Wa Swawm Na Kufungua Kutokana Tofauti Ya Mwandamo Wa Mwezi

 

Hilaal: Waislamu Wote Duniani Wafuate Mwandamo Mmoja Wafunge Na Kula ‘Iyd Siku Moja ?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share