Huhisi Kuongea Akilini Mwake na Uchukivu wa Mtu Kumuongelesha Je Ni Uchawi?

 

Huhisi Kuongea Akilini Mwake na Uchukivu

wa Mtu Kumuongelesha Je Ni Uchawi?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI: 

 

Nashukru Alhidaya Kwa Kutuelimish, Allah Awazidishiye Kama Nataka Maswahili Yangu Minitumiye Ndani Ya E-mail Yangu. Je Munaweza, If Yes, Jazakalahukhaira,

Swahi langu ni,   kila wakati asubuhi hadi nalala naona mambo ngeni katika akilini mwangu naona kama niko hapo na saa ingine naongeya. Kila wakati mtu akiniongelesha nachukiya mtu akiniongelesha.  Sasa sijuwi kama huu ni uchawi.

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Hakika hii huenda ikawa ni hisia yako tu ambayo inajitokeza kwa kuwa na uchukivu wa aina hiyo uliyoitaja. Jambo lako wewe kufanya ni kujaribu sana kusoma Qur-aan kila siku na Adhkaar za asubuhi na usiku ambazo zipo kaitika viungo vifuatavyo:

 

 

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi kuhusu kujikinga na shari kama hizo:

 

Kuhusu Mashaytwaan Na Vipi Kujikinga Nao

 

Kujikinga Na Ushirikina Wa Uchawi Na Mauaji

 

Kufanya hivyo tunatarajia kuwa hisia hizo huenda zikaondoka.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

Share