Shaykh Fawzaan - Utamjuaje Mtu Wa Matamanio (Bid'ah)?

Utamjuaje Mtu Wa Matamanio?

 

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu-Allaah) amesema:

“Utakapomwambia mtu wa Haki pindi anapokosea: ‘Umekosea dalili, umekosea Sunnah’. Basi atakubali (kukosolewa) kwa sababu yeye anakusudia Haki, na wala si lengo lake kushinda kwa rai yake.

 

Ama utakapomwambia mtu wa Matamanio (bid’ah): ‘Umekosea’. Basi utamuona anakasirika na anakuwa mkali. Na hii ni alama ya watu wa matamanio (bid’ah). Kila mmoja wao hutaka kushinda kwa ajili ya matamanio yake.”

 

 

[Sharh As-Sunnah Lil-Barbahaariy, uk. 56]

 

Share