Skip to main content

Majina Ya Allaah Mazuri Na Sifa Zake: أَسْمَآءُ اللهِ الحُسْنَى وَصِفَاتُهُ (Tafasili, Taathira, Faida Na Mafunzo)Faharasa: Mukhtasari Wa Majina Ya Allaah Mazuri Na Sifa Zake: أَسْمَآءُ اللهِ الحُسْنَى وَصِفَاتُهُ

Faharasa / Mukhtasari Rudi kwenye Orodha ya Majina
Faharasa: Mukhtasari Wa Majina Ya Allaah

Na.

Jina / Sifa

Tamshi

Maana

1

الله

Allaah

Mwenye Uluwhiyyah; Muabudiwa wa haki Pekee, Anayestahiki kuabudiwa na viumbe vyote bila kushirikishwa na yeyote.

2

الإله

Al-Ilaah

Muabudiwa wa haki (Ilaah); Anayestahiki kuabudiwa Pekee.

3

الرّب

Ar-Rabb

Rabb wa kila kitu: Mola, Bwana, Muumbaji, Mmiliki, Mfalme, Mwenye Kuruzuku, Mlezi, Msimamizi, Mneemeshaji na Mwendeshaji wa mambo yote.

4

الرّحمن

Ar-Rahmaan

Mwingi wa Rehma; Mwenye Rehma pana iliyoenea viumbe vyote.

5

الرّحيم

Ar-Rahiym

Mwenye Kurehemu; Mwenye Kuwafikishia Waja Wake Rehma Yake, na khaswa Rehma makhsusi kwa Waumini duniani na Aakhirah.

6

الحيّ

Al-Hayy

Aliye Hai daima; Mwenye uhai kamili usiotanguliwa na kutokuwepo, wala usiofikwa na kutoweka.

7

القيّوم

Al-Qayyuwm

Msimamizi wa kila kitu; Aliyesimama kwa Dhati Yake bila Kumhitajia yeyote, na Anayesimamia mambo ya viumbe Vyake vyote, kila kitu kinamhitajia Yeye.

8

الصّمد

Asw-Swamad

Bwana Aliyekamilika katika ubwana na Utukufu Wake, Anayekusudiwa na viumbe wote kwa haja zao zote, Naye Hamhitajii yeyote.

9

الأوّل

Al-Awwal

Wa Awali Ambaye hakuna kitu chochote kabla Yake; Aliyekuwepo bila ya mwanzo.

10

الآخر

Al-Aakhir

Wa Mwisho Ambaye hakuna kitu chochote baada Yake; Mwenye Kubakia daima baada ya kutoweka kwa kila kiumbe.

11

الظّاهر

Adhw-Dhwaahir

Aliye juu kabisa, hakuna kitu juu Yake; Aliyeshinda kila kitu, na Aliyedhihirika kwa Dalili Zake.

12

الباطن

Al-Baatwin

Aliye karibu, hakuna kitu kilicho karibu kuliko Yeye kwa Ujuzi Wake; Mjuzi wa ya ndani ya kila kitu, Aliyefichikana na macho ya viumbe duniani.

13

الواحد

Al-Waahid

Mmoja Pekee Asiye na kifano; Mmoja Pekee kwa Dhati Yake na Sifa Zake.

14

الأحد

Al-Ahad

Mmoja Pekee, Hana mshirika; Hakuzaa wala Hakuzaliwa, wala hakuna yeyote anayefanana Naye.

15

الملك

Al-Malik

Mfalme na Mwenye mamlaka kamili juu ya viumbe vyote; Mwenye Kuamrisha na Kukataza, na Kuyaendesha mambo yote Apendavyo.

16

المالك

Al-Maalik

Mwenye Kumiliki kila kitu; ufalme wote ni Wake, Anampa Amtakaye na Anamuondoshea Amtakaye.

17

المليك

Al-Maliyk

Mfalme Mwenye ufalme mkamilifu, Mwenye nguvu zote daima.

18

القدّوس

Al-Qudduws

Mtakatifu; Aliyetakasika na kila aina ya upungufu, kasoro na aibu, Mwenye Kustahiki kutukuzwa na kutakaswa, Mwingi wa baraka.

19

السّلام

As-Salaam

Aliyesalimika na kila aibu, kasoro na upungufu; Mwenye Kuwasalimisha Waja Wake, na Chanzo cha kila amani na usalama.

20

المؤمن

Al-Muumin

Mwenye Kusadikisha Ahadi Zake; Mwenye Kuwapa Waja Wake amani na usalama.

21

المهيمن

Al-Muhaymin

Mwenye Kushuhudia, Kuchunga, Kudhibiti na Kuhifadhi; Mjuzi wa yaliyofichikana, Mwenye Kuendesha mambo ya viumbe Vyake.

22

العزيز

Al-‘Aziyz

Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika; Mwenye ‘izzah (utukufu na nguvu) zote, Asiyefikiwa wala Asiyedhurika.

23

الجبّار

Al-Jabbaar

Jabari; Mwenye Kuunga na Kurekebisha kilichovunjika, Mwenye Kudhibiti viumbe vyote, Aliye juu Asiyeshindwa Kufanya Atakalo.

24

المتكبّر

Al-Mutakabbir

Mwenye Ukubwa na Utukufu wote; Aliyetakasika na kila aibu, dhulma na upungufu.

25

الخالق

Al-Khaaliq

Muumbaji; Aliyeviumba viumbe vyote kutoka kutokuwepo, na Akakikadiria kila kitu makadirio kamili; Yeye Ndiye Muumbaji wa kila kitu.

26

الخلاّق

Al-Khallaaq

Mwingi wa Kuumba; Anayeumba mara kwa mara Atakavyo na Anavyotaka, Muumbaji wa kila namna kwa wingi.

27

البارئ

Al-Baariu

Mwanzilishi wa viumbe; Mwenye Kutekeleza na Kuleta katika uhai yale Aliyoyakadiria bila ya kasoro, na Kuvipambanua viumbe kila kimoja na umbo lake.

28

المصوّر

Al-Muswawwir

Muundaji wa sura na maumbo; Ambaye Ameunda sura za viumbe vyote kama Atakavyo, na Akakipa kila kimoja sura yake maalumu.

29

الحكم

Al-Hakam

Mwamuzi; Anayehukumu baina ya viumbe Vyake kwa uadilifu bila Kumdhulumu yeyote, na Aliyeteremsha Kitabu Chake kiwe hakimu baina ya watu.

30

الحكيم

Al-Hakiym

Mwenye Hikmah wa yote; Mwenye Kuweka kila kitu mahali pake, Ambaye Maneno Yake, Matendo Yake na Hukumu Zake zote ni haki, uadilifu na usahihi.

31

السّميع

As-Samiy’

Mwenye Kusikia yote daima; Ambaye Usikivu Wake umeenea kila sauti, ya siri na ya dhahiri, na Anayesikia na Kuitikia du’aa za Waja Wake.

32

البصير

Al-Baswiyr

Mwenye Kuona yote; Ambaye Kuona Kwake kumezunguka kila kinachoonekana, kidogo na kikubwa, cha dhahiri na cha siri.

33

العليم

Al-‘Aliym

Mjuzi wa yote; Ambaye Ujuzi Wake umekizunguka kila kitu, cha dhahiri na cha siri, kilichopita, kilichopo na kitakachokuja.

34

القريب

Al-Qariyb

Aliye karibu na Waja Wake kwa Ujuzi Wake, Kusikia Kwake na Kuona Kwake, na karibu na wanaomwomba kwa Kuwaitikia; pamoja na kuwa Yuko juu ya ‘Arsh Yake.

35

المجيب

Al-Mujiyb

Mwenye Kuitikia; Anayeitikia du’aa za wanaomwomba, Anayemjibu mwenye shida, na Anayewapa Waja Wake wanachokiomba kwa mujibu wa Hikmah Yake.

36

العفوّ

Al-‘Afuww

Mwingi wa Kusamehe; Anayefuta madhambi ya Waja Wake na Kuyaondoa athari zake, wala Hawaadhibu kwayo.

37

الغفور

Al-Ghafuwr

Mwingi wa Kughufuria; Anayesitiri madhambi ya Waja Wake na Kuwaepusha na Adhabu Yake.

38

الغفّار

Al-Ghaffaar

Mwingi mno wa Kughufuria; Anayeghufuria madhambi ya Waja Wake mara baada ya mara, kila wanaporudi Kwake.

39

التواب

At-Tawwaab

Mwingi wa Kupokea tawbah; Anayewawafikisha Waja Wake kutubia, kisha Anapokea tawbah yao mara baada ya mara.

40

الرّؤوف

Ar-Rauwf

Mwenye huruma mno; Ambaye Huruma Yake kwa Waja Wake ni kubwa, laini na ya kuwaepusha na kila madhara.

41

البرّ

Al-Barr

Mwingi wa wema na ihsaan; Ambaye Wema Wake umewaenea viumbe Vyake vyote, na Anawafanyia Waumini wema maalumu duniani na Aakhirah.

42

الْعَلِيُّ

Al-‘Aliyy

Aliye juu kabisa; Mwenye ‘Uluwa wa Dhati Yake juu ya viumbe Vyake, ‘Uluwa wa Utukufu na hadhi, na ‘Uluwa wa Kushinda na Kudhibiti kila kitu.

43

الأعلى

Al-A’laa

Aliye juu kuliko kila kitu; Ambaye hakuna aliye juu Yake, wala Hana mfano katika Sifa Zake za juu.

44

الرّازق

Ar-Raaziq

Mwenye Kuruzuku; Anayewapa rizqi viumbe wote, Amezipanga rizqi zao kabla ya Kuwaumba, na Amedhamini Kuzikamilisha.

45

الرّزاق

Ar-Razzaaq

Mwingi wa Kuruzuku; Anawaruzuku viumbe kabla ya wao kumuomba, na Anawaruzuku hata pale wanapomuasi.

46

الفتّاح

Al-Fattaah

Mwingi wa Kufungua na Hakimu; Anayefungua Atakacho katika hazina za Ufalme Wake, Rehma Zake na Rizqi Zake, na Anayehukumu baina ya Waja Wake kwa haki.

47

الحفيظ

Al-Hafiydhw

Mwenye Kuhifadhi; Aliyehifadhi Alichokiumba, na Akawahifadhi Awliyaa Wake wasitumbukie katika madhambi na maangamizi, na Amewadhibitia waja amali zao na Atawalipa kwazo.

48

الودود

Al-Waduwd

Mwenye mapenzi halisi; Mwenye Kuwapenda Awliyaa Wake na wanaorejea Kwake kwa tawbah, Anawadhihirishia Mapenzi Yake kwa maghfirah na Neema Zake, na Mwenye kupendwa na Waja Wake.

49

الولي

Al-Waliyy

Walii; Mwenye Kuyatawalia mambo ya Waja Wake na Kuyasimamia, Mwenye Kuwapenda, Kuwalinda, Kuwanusuru na Kuwaneemesha Waumini.

50

المولى

Al-Mawlaa

Maulaa; Bwana Mlezi, Msaidizi na Mlinzi Anayetarajiwa kwa nusura na msaada; Yeye Pekee Ndiye Mbora wa Kulinda na Kunusuru.

51

المتين

Al-Matiyn

Mwenye nguvu shadidi; Ambaye Nguvu Zake hazidhoofiki, wala Hapatwi na mashaka wala taklifa wala uchovu katika Matendo Yake.

52

الغني

Al-Ghaniyy

Mkwasi, Asiyehitaji kitu; Hamhitajii kiumbe Wake yeyote kwa Ukamilifu Wake na ukamilifu wa Sifa Zake, na viumbe vyote vinamhitajia Yeye, Neema Zake na Msaada Wake.

53

الكريم

Al-Kariym

Karimu; Mwingi wa kheri na Kutoa, Anatoa Anachotaka Kumpa Amtakaye, kwa namna Atakayo, kwa kuombwa na bila ya kuombwa.

54

الأكرم

Al-Akram

Aliyefikia ukomo wa ukarimu; Mkarimu kuliko wakarimu wote, Hana wa kufanana Naye katika hilo wala wa kulingana Naye.

55

اللّطيف

Al-Latwiyf

Latifu; Mjuzi wa mambo ya ndani, Kwake halijifichi lenye kujificha, na Anawafikishia Waja Wake kheri na manufaa kwa njia zilizofichika na kwa upole.

56

الخبير

Al-Khabiyr

Mjuzi wa undani wa mambo; Ambaye Ujuzi Wake umevizunguka vitu vya ndani na vilivyofichika kama ulivyovizunguka vya dhahiri.

57

الحليم

Al-Haliym

Mpole Mwenye Kuwavumilia Waja Wake; Ambaye Haharakishi Kuwaadhibu Waja Wake.

58

العظيم

Al-‘Adhwiym

Adhimu; Mwenye Kusifika kwa utukufu, Mwenye Taadhima, Mkubwa na Mkuu kabisa Aliyetukuka, Mwenye Ujalali na Ukarimu.

59

الحميد

Al-Hamiyd

Msifiwa, Mwenye kushukuriwa kwa yote daima; Mwenye kuhimidiwa na Kustahiki Himdi kwa Matendo Yake kwa viumbe Vyake, kwa Neema na Fadhila Alizowapa.

60

الشّاكر

Ash-Shaakir

Mwenye Kupokea shukurani; Anamsifu anayemtii, na Anampa thawabu kwa utiifu wake.

61

الشكور

Ash-Shakuwr

Mwingi wa Kupokea shukurani; Ambaye amali ndogo za waja hukua Kwake, na Huwarudufishia malipo.

62

المقيت

Al-Muqiyt

Mwenye Uwezo, Mwenye Kudhibiti, Mwenye Kuhifadhi, Mwangalizi na Mwenye Kuwapa viumbe chakula chao.

63

الحسيب

Al-Hasiyb

Mwenye Kuhesabu, Mwenye Kutosheleza, Mwenye Kuhifadhi na Mwenye Kushuhudia; Anayewatosheleza Waja Wake, na Atawahesabu kwa amali zao.

64

المحيط

Al-Muhiytw

Mwenye Kuzunguka kila kitu; Ambaye Ujuzi Wake, Uwezo Wake na Mamlaka Yake vimekizunguka kila kitu.

65

الرقيب

Ar-Raqiyb

Mwenye Kuchunga; Mwenye Kusifika kwa Kuchunga na Kuhifadhi, na Kuangalia kwa makini; hakuna kinachofichika Kwake.

66

المجيد

Al-Majiyd

Mwenye Utukufu kamili; Anayestahiki fahari, ukarimu, utukufu na hadhi ya juu mbinguni na ardhini, Mwingi wa vipawa na ukarimu.

67

الشّافي

Ash-Shaafiy

Mwenye Kuponyesha; Anayeponya magonjwa ya miili na nyoyo, hakuna shifaa isipokuwa Shifaa Yake.

68

الشهيد

Ash-Shahiyd

Shahidi; Mwenye Kujua vyema yanayoonekana na yaliyofichika, Mwenye Kushuhudia kila kitu.

69

الوكيل

Al-Wakiyl

Mtegemewa kwa yote, Mdhamini na Msimamizi; Anayetegemewa na Waja Wake, Anayesimamia mambo yao yote na Kuwatosheleza.

70

القوي

Al-Qawiyy

Mwenye nguvu zote daima; Ambaye Nguvu Zake ni kamilifu, hakuna kinachomshinda wala kumdhoofisha.

71

الكبير

Al-Kabiyr

Mkubwa kabisa; Ambaye kila kitu ni kidogo mbele ya Ukubwa Wake, katika Dhati Yake, Sifa Zake na Matendo Yake.

72

المتعال

Al-Muta’aal

Aliyetukuka juu ya kila kitu; Aliyejitakasa na Kuwa mbali kabisa na kila upungufu, na kila wanalomnasibishia washirikina.

73

الجواد

Al-Jawaad

Mwingi wa ukarimu; Mwenye Kutoa kwa wingi bila kikomo, Ambaye Ukarimu Wake umewaenea viumbe vyote.

74

الحفي

Al-Hafiyy

Mwenye Kuwahurumia sana na Kuwajali Waja Wake; Mwenye Kuwafanyia wema na upole na Kuwaitikia.

75

الوارث

Al-Waarith

Mrithi; Atakayebaki baada ya kutoweka viumbe vyote, na kila kitu kitarejea Kwake.

76

القادر

Al-Qaadir

Muweza; Ambaye Ana uwezo kamili juu ya kila kitu, hakuna kinachomshinda.

77

القدير

Al-Qadiyr

Muweza wa yote; Mwenye Uwezo mkamilifu na mwingi juu ya kila kitu, hakuna kinachomshinda.

78

المقتدر

Al-Muqtadir

Mwenye Uwezo uliokamilika kabisa; Ambaye Uwezo Wake unadhihirika katika Kuwakamata madhalimu na Kutekeleza Analolitaka bila ya kizuizi.

79

القاهر

Al-Qaahir

Mwenye Kudhibiti na Kushinda; Aliyedhibiti vyote chini ya Mamlaka Yake, Aliye juu ya Waja Wake, hakuna kinachoweza kumpinga.

80

القهّار

Al-Qahhaar

Mwenye Kudhibiti kila kitu kwa ukamilifu; Ambaye viumbe vyote vimemnyenyekea, na majabari wote wamedhalilika mbele Yake.

81

الحق

Al-Haqq

Haki; Ambaye Kuwepo Kwake ni kwa kweli kusikoweza kukanushwa, Maneno Yake ni kweli, Ahadi Yake ni kweli, na ‘ibaadah ya kweli ni Yake Pekee.

82

المبين

Al-Mubiyn

Aliye wazi, Ambaye hakuna shaka katika Uluwhiyyah Yake na kustahiki Kwake ‘Ubuwdiyyah (kuabudiwa); na Mwenye Kubainisha waziwazi njia ya uongofu na njia ya upotofu kwa Waja Wake.

83

الواسع

Al-Waasi’

Mwenye wasaa; Ambaye Sifa Zake ni pana zisizo na mipaka: Ujuzi Wake, Rehma Yake, Maghfirah Yake na Fadhila Zake zimeenea kila kitu.

84

الوهّاب

Al-Wahhaab

Mwingi wa Kutunuku; Anayetoa zawadi na neema nyingi bila kuombwa badala, na bila kukoma wala kupungua kwa Hazina Zake.

85

الهادي

Al-Haadiy

Mwenye Kuongoza; Anayewaongoza viumbe Vyake kwenye maslahi yao, na Anayewaongoza Waumini kwenye njia iliyonyooka.

86

النصير

An-Naswiyr

Mwenye Kunusuru; Anayewasaidia na Kuwanusuru Waumini dhidi ya maadui zao, na hakuna wa kumshinda Anayemnusuru.

87

الكافي

Al-Kaafiy

Mwenye Kutosheleza; Anayewatosheleza Waja Wake katika kila wanachokihitaji, na Anayewalinda na shari ya maadui zao.

88

الرّفيق

Ar-Rafiyq

Mpole; Mwenye upole katika Matendo Yake na Sharia Zake, Anayependa upole, na Anayetoa kwa upole yale Asiyoyatoa kwa ukali.

89

الجميل

Al-Jamiyl

Mzuri; Mwenye uzuri kamili katika Dhati Yake, Majina Yake, Sifa Zake na Matendo Yake, na Anayependa uzuri.

90

القابض

Al-Qaabidhw

Mwenye Kubana na Kushika; Anayebana rizqi kwa Amtakaye kwa Hikmah Yake, na Anayeshika roho za viumbe.

91

الباسط

Al-Baasitw

Mwenye Kukunjua; Anayekunjua rizqi kwa Amtakaye, Anayekunjua Mkono Wake Kupokea tawbah, na Anayekunjua nyoyo kwa furaha na imaan.

92

المعطي

Al-Mu’twiy

Mwenye Kutoa; Anayetoa kila neema kwa viumbe Vyake, Anayempa Amtakaye kwa Hikmah Yake, wala hakuna wa kuzuia Alichokitoa.

93

المقدّم

Al-Muqaddim

Mwenye Kutanguliza; Anayetanguliza Amtakaye na Akitakacho kwa Hikmah Yake, katika uumbaji, katika daraja na katika fadhila.

94

المؤخّر

Al-Muakh-khir

Mwenye Kuakhirisha; Anayeakhirisha Amtakaye na Akitakacho kwa Hikmah Yake, Anayewapa madhalimu muda, na Anayeakhirisha adhabu ili waja watubie.

95

المنّان

Al-Mannaan

Mwingi wa Kuneemesha; Anayetoa neema kubwa bila ya kuombwa wala Kutarajia malipo, na Mwenye Kustahiki Kuzitaja Neema Zake juu ya Waja Wake.

96

السّيّد

As-Sayyid

Bwana; Mwenye ubwana kamili juu ya viumbe vyote, Aliyekamilika katika Utukufu Wake, Anayerejewa na viumbe vyote katika haja zao.

97

الحيي

Al-Hayiyy

Mwenye haya; haya inayolingana na Utukufu Wake, isiyofanana na haya ya viumbe; Anayependa haya, na Anaona haya Kuirudisha mikono ya Mja Wake mitupu.

98

السِّتِّير

As-Sittiyr

Mwingi wa Kusitiri; Anayesitiri aibu na madhambi ya Waja Wake wala Hawaumbui, na Anayependa sitara.

99

الوتر

Al-Witr

Mmoja Asiye na mwenzi; Witiri katika Dhati Yake, Sifa Zake na Matendo Yake, Asiye na mfano wala mshirika, na Anayependa witiri.

100

المحسن

Al-Muhsin

Mwenye Kufanya ihsaan; Mwenye Kuwafanyia wema viumbe Vyake kwa fadhila zinazozidi uadilifu, na Aliyetengeneza kwa umahiri kila kitu Alichokiumba.

101

الطّيّب

At-Twayyib

Mzuri, Msafi, Aliyetakasika na kila upungufu na aibu; Mzuri katika Dhati Yake, Majina Yake, Sifa Zake, Matendo Yake na Hukumu Zake, Asiyekubali isipokuwa kilicho kizuri.

102

السُّبُّوح

As-Subbuwh

Mwingi wa kutakaswa; Aliyetakasika na kila aibu, kila upungufu, mshirika, mke na mwana, na kila kisicholingana na Uluwhiyyah Yake.

103

الحافظ

Al-Haafidhw

Mwenye Kuhifadhi; Anayehifadhi viumbe Vyake, Anayewahifadhi Waja Wake na shari, maovu na balaa, na Anayehifadhi amali za waja bila ya kupotea chochote.

Majina Yaliyokuja Kwa Kuunganishwa (Mudhwaaf)

Haya ni Majina yaliyokuja yakiunganishwa (yakiegemezwa) na neno jengine katika Qur-aan, na hutajwa kwa sura hiyo kama yalivyokuja. Yameandikwa hapa kwa maneno yake ya Qur-aan pamoja na Tarjama yake.

Tanbihi: Baadhi ya ‘Ulamaa wanayahesabu baadhi ya haya kuwa ni Sifa za Allaah zilizokuja kwa kuunganishwa kuliko kuwa ni Majina; lakini haya ndiyo yanayotajwa zaidi na kukubaliwa na ‘Ulamaa wengi.

Maneno Ya Qur-aan

Tarjama Yake

رَبِّ الْعَالَمِينَ

Rabb wa walimwengu.

Rejea: Al-Faatihah (1:2); Al-An’aam (6:162).

مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ

Mfalme wa Siku ya Malipo.

Rejea: Al-Faatihah (1:4).

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

Mbunifu wa mbingu na ardhi (bila ya mfano uliotangulia).

Rejea: Al-Baqarah (2:117); Al-An’aam (6:101).

جَامِعُ النَّاسِ

Mkusanyaji watu (Siku isiyo na shaka ndani yake).

Rejea: Aal-‘Imraan (3:9).

مَالِكَ الْمُلْكِ

Mfalme Uliyemiliki ufalme wote.

Rejea: Aal-‘Imraan (3:26).

فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

Mwanzilishi wa mbingu na ardhi.

Rejea: Al-An’aam (6:14); Ibraahiym (14:10); Faatwir (35:1).

عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ

Mjuzi wa ghaibu na dhahiri.

Rejea: Al-An’aam (6:73); Al-Hashr (59:22).

فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ

Anafanya Atakavyo; Mwingi wa Kufanya Atakalo.

Rejea: Huwd (11:107); Al-Buruwj (85:16).

نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

Nuru ya mbingu na ardhi.

Rejea: An-Nuwr (24:35).

ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ

Mwenye Ujalali na Ukarimu.

Rejea: Ar-Rahmaan (55:27).

Na Allaah Mjuzi zaidi